Latest News


More

Posted on : Friday, November 26, 2010 [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila

Hayawi hayawi hatimae yamekua .likua ni siku njema na ya tulivu kwa bwana Juma Kanena baada ya kufunga pingu za maisha al maarufu kama kupata mke au wengine wanasema kupata jiko.Shughuli hii ilifanyika nyumbani kwa wakwe zake huko Mbagala Charambe na baadaye mnuso wa nguvu ulifanyika katika hoteli ya Paradise iliyoko katika jengo la Benjamen Mkapa .Mnuso huu ulikua ni kwa marafiki na ndugu wa karibu kama inavyoonyesha kwenye picha hapo juu.Bwana Juma ni mfanyakazi wa Wizara ya mambo ya ndani na mke wake ni mwalimu.Big up Juma
Posted on : Thursday, November 25, 2010 [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Wazazi wa Evaresta Livingstone Kisanga na mke wake wakiwa katika picha ya pamoja
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Evaresta akiwa na mpambe wake tayari kufungua shampaigne.Hakika walipendeza

Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila

Wadhamini wa Evaresta wakiwa nao wamekaa kwa pamoja kwenye sherehe hiyo.Wadhamini ni baba yake mdogo Ronald na shangazi yake.Big Up!!
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Jumapili iliyopita ilikua siku nzuri sana kwa binti wa Livingstone Kisanga wa Mbezi juu.Siku hii binti huyu anayeitwa Evaresta alipata Kipaimara katika kanisa la Mbezi jyy K.K.K.T.Pichani akiwa na mpambe wake Esta Kisanga wakiwa wamekaa meza kuu tayari kuanza kwa sherehe hiyo.Sherehe hii ilifanyika nyumbani kwao Mbezi juu.Wana blog tunamtakia kila laheri na baraka tele.Mungu amsaidie aendelee kukua kiroho.Amen
Posted on : Wednesday, November 24, 2010 [0] comments Label: ,

BARAZA LA MAWAZIRI JIPYA TANZANIA LATAJWA

by : Tumaini Kichila
BARAZA LA MAWAZIRI JIPYA NOVEMBA, 2010 LATANGAZWA RASMI…!!!

MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI
NA.
OFISI/WIZARA
WAZIRI
NAIBU WAZIRI

1.
Ofisi ya Rais
WN – OR – Utawala Bora
Mathias Chikawe
WN – OR – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira

2.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Hawa Ghasia

3.
Ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano
Samia Suluhu

Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa
4.
Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi
Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu

5.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
George Huruma Mkuchika
1.Aggrey Mwanri
2. Kassim Majaliwa


6.
Wizara ya Fedha
Mustapha Mkulo
1. Gregory Teu
2. Pereira Ame Silima


7.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Shamsi Vuai Nahodha
1. Balozi Khamis Suedi Kagasheki


8.
Wizara ya Katiba na Sheria
Celina Kombani

9.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard K. Membe
1. Mahadhi Juma Mahadhi


10.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

11.
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. Mathayo David Mathayo
1. Benedict Ole Nangoro


12.
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
1. Charles Kitwanga


13.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka
Goodluck Ole Madeye


14.
Wizara ya Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige

15.
Wizara ya Nishati na Madini
William Mganga Ngeleja
1. Adam Kigoma Malima


16.
Wizara ya Ujenzi
Dr. John Pombe Magufuli
1. Dr. Harrison Mwakyembe


17.
Wizara ya Uchukuzi
Omari Nundu
1. Athumani Mfutakamba


18.
Wizara ya Viwanda na Biashara
Dr. Cyril Chami
Lazaro Nyalandu


19.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru Kawambwa
1. Philipo Mulugo


20.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Haji Hussein Mpanda
1. Dr. Lucy Nkya


21.
Wizara ya Kazi na Ajira
Gaudensia KabakaMakongoro Mahanga

22.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Sophia Simba
Umi Ali Mwalimu


23.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo
Emmanuel John Nchimbi1. Dr. Fenella Mukangara

24.
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Samuel John Sitta
1. Dr. Abdallah Juma Abdallah


25.
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Prof. Jumanne Maghembe
1. Christopher Chiza


26.
Wizara ya Maji
Prof. Mark James MwandosyaEng. Gerson Lwinge
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Mdau na shemeji yake Ferdy Bwojo
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Mdau akiwa na watoto wa dada yake, Sarah kushoto na Noely kulia
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Picha ya pamoja na wanafamilia.Toka kushoto ni mtoto wa dada yake Sarah, dada yake Elinipa, my wife wake Lilian, na shemeji yake Rogzena.Nyuma aliyevaa shati jeusi ni mdogo wake Jackson.Anayechungulia nyuma ni mtoto wa dada yake Noely
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila
Mdau akiwa na dada yake

Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila

Mdau akiwa katika poz na my wife wake
Posted on : [0] comments Label: ,

by : Tumaini Kichila

Mdau akiwa nabaadhi ya ndugu zake pamoja na chei alichotunukiwa cha mwanafunzi bora wa kozi ya Postgraduate Diploma kwa somo la Strategy Management
Posted on : [0] comments Label: ,

Mahafali CBE

by : Tumaini Kichila

Jumamosi iliyopita tarehe 20/11/2010 chuo cha CBE kilifanya mahafali yake ya 45.Mmojawapo wa wadau waliograduate siku hiyo ni mdau wa blog hii Tumaini Kichila ambaye alipata Postgraduate Diploma ya Business Administration (sijui kiswahili chake ni nini)
Pichani mdau akiwa na my wife wake katika pozi Lilian Regis.Makofi kwake tafahali.Picha zaidi kama zinavyoonekana hapo juu
Posted on : Friday, November 5, 2010 [0] comments Label: ,

JUBILEE YA MWAKA YAFANYIKA MOSHI MJINI

by : Tumaini Kichila

Harusi ya nguvu ilifanyika mwishoni mwa mwezi wa kumi huko mjini Moshi kati ya Bwana na Bibi Rangia Mushi.Maharusi hawa walifanya Jubilee ya ndoa yao ya kutimiza miaka 50 tangu wafunge ndoa yao kwa mara ya kwanza.Ilikua harusi ya kufana na ilihudhuriwa na ndugu na marafiki wa karibu wa familia hii na ilifanyika katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Majengo mjini Moshi
Picha ya juu ikionyesha maharusi hao baada ya kutoka kanisani.
Hakika maharusi hawa walimeremeta sana
Ni jambo la kumshukuru sana Mungu kutimiza miaka 50 ndani ya ndoa.Shukrani za pekee ziwaendee watoto wa maharusi hawa ambao ndio waliofanikisha harusi na sherehe ya wanandoa hawa, wakiongozwa na Dr.Allen Mushi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam .Hakika mlifanya jambo la kukumbukwa na la baraka mbele za Mungu
Tunawatakia kila la heri maharusi hawa na Mungu awajalie maisha mema ya baraka tele
Amina!!
Maharusi wakiwa katika ukumbi wa sherehe.

Maharusi wakiwa tayari kupata picha ya kumbukumbu katika mzunguko wa kuelekea Arusha ambapo ni mahali maarufu sana kwa picha mjini Moshi

Picha juu maharusi baada ya kutoka kanisani wakiwa na watoto wapambaji wa harusi yao.Watoto hawa wadogo walikua ni wajukuu wa maharusi hao.


Gari lililotumika kubeba maharusi.Hakika watoto wa maharusi hao walijiandaa sawa sawa kuwapamba wazazi wao na kuhakikisha wanatoka bomba.Hongera sana Dr.Allen Mushi kwa kazi nzuri


Maharusi wakiwa na wapambe wao baada ya kutoka kanisani
Maharusi wakiwa kwenye tabasamu la nguvu.
Hongereni sana Bwana na Bibi Rangia Mushi
Posted on : Thursday, November 4, 2010 [0] comments Label: ,

Wabunge watano machachari

by : Tumaini Kichila
Wakati matokeo ya uchaguzi yakielekea ukingoni kutoka bunge lwa mwaka huu au la awamu hii linatua na sura mpya nyingi.Kati ya wabunge wateule ambao nadhani watatia chachu sana katika vikao vya bunge hapo Dodoma ni hawa wafuatao hapa chini
1.Halima Mdee wa Chadema
2.Mama Tibaijuka wa CCM
3.Bwana Mnyika wa Chadema
4.Mr Lyatonga Mrema wa TLP
5.Mr Mbilinyi (aka sugu) wa Chadema


Juu ni picha ya Halima Mdee wa Chadema mmojawapo wa mbunge kijana machachari wa Chadema.Huyu alikuwa kwenye bunge lililopita kama mwakilishi wa kuteuliwa.Lakini Mdee mwaka huu kaamua kusimama na kupigana na ameaonyesha hana sababu ya kusubiri viti vya kuteuliwa ila anaweza kusimama mwenyewe na kupambana hadi ushindi
I like it...Keep it up dada yangu

Mama Tibaijuka.Huyu mama hakuna asiyemjua jinsi alivyokua anapambana na mambo ya makazi.Kipindi cha vurugu za uchaguzi huko Kenya alisimama kidete kuwatetea wale ambao walivunjiwa nyumba zao.Nadhani atakua na mchango mkubwa katika nchi yetu


Bwana Mbilinyi aka sugu.Huyu ni mwanaharakati na mpiganaji halisi wa maswala ya unyanyasaji na kudai haki.Huyu bwana yuko radhi kuhatarisha usalama wake mradi tu apate haki yake.Wengi mtamkumbuka na album yake ya ant virus.Hii album inazungumzia haki za wasanii zinavyoibiwa.
Nadhani wasanii sasa mmepata mwakilishi wenu bungeni
Tunakutakia kila la heri


Bwana Mnyika mmojawapo wa wabunge vijana wa bunge linalokuja.Kijana huyu naye ni mwanaharakati wa kutetea wanyonge na haswa vijana wasio na ajira.Nadhani naye ana mchango mkubwa sana katika bunge letu linalokuja
Kila la heri kaka


Bwana Lyatonga Mrema.Huyu hakuna asiye mjua katika nchi yetu.Amekua mmojawapo wa viongozi wa upinzania alieyeleta changamoto sana katika mageuzi hapa nchini.Amewahi kutumikia NCCR Mageuzi na sasa yuko TLP kama mbunge wa Vunjo.
Mchango wake bado tunaukumbuka akiwa waziri wa mambo ya ndani
Tunakutakia kila la heri baba