Latest News


More

JE UNAWAJUA WAYAHUDI?

Posted by : Unknown on : Friday, May 31, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,



JE UNAWAJUA WAYAHUDI?

Jina la Wayahudi halikutumiwa katika Agano la Kale kabla ya kugawanywa ufalme wa Israel.Baada ya kufa kwake Sulemani ufalme uligawanywa katika sehemu mbili, yaani sehemu ya Kaskazini iliyoitwa Israel na sehemu ya Kusini iliyoitwa Yuda.

Ingawa watu wa ufalme wa kusini walikuwa Waisraeli kwa damu (kwa sababu wao pia walikuwa wazao wa Yakobo, au Israeli),waliitwa Wayuda ili kuwatofautisha na watu wa ufalme wa Kaskazini.Baadaye waliitwa Wayahudi (Yeremia 34:9)

Baadaye falme zote mbili ziliangamizwa, na watu wake walipelekwa kifungoni katika nchi za kigeni.Halafu wazao wa wafungwa wale waliporuhusiwa kurudi katika nchi yao ya Israel, wengi wao waliporudi walikuwa wale wa ufalme wa kusini, yaani Wayahudi.

Wakati ule jina la Wayahudi lilitumiwa kila mahali na kwa wote walioishi katika nchi yao ya zamani wakati huo, pasipo kutaja kabila la asili yao.Kwa maneno mengine ,jina lile lilitumiwa kwa Waisrael wote.(Ezra 6:7;Neh 6:6;Dan 3:8)

Wakati wa Agano Jipya majina ya Waebrania,Waisrael na Wayahudi yalitumiwa kwa kuchanganywa  
(Mt 2:2;Yn 1:19;2Kor 11:22; 1 Kor 9:20;Flp 3:5;Rum 1:16

(Imeandaliwa na Kichila  - 2003)

No comments:

Leave a Reply