Latest News


More

KANTATE DOMINO YAFANA KANISA LA K.K.K.T USHARIKA WA MAKONGO

Posted by : Unknown on : Thursday, May 23, 2013 0 comments
Unknown
 Sikukuu ya Kantate Domino (Mwimbieni Bwana wimbo mpya) ilifana katika Usharika wa Makongo ambapo baadhi ya kwaya za Jimbo la Kaskazini la Kanisa la Kiinjili  la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Mashariki na Pwani zilikutana kumwimbia bwana.

Baadhi ya kwaya hizi ni kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge.Pichani juu na chini wanakwaya wa kwaya hiyo wakipanda jukwaani tayari kumwimbia bwana
 Aliyevaa kola ya Kichungaji ni mchungaji wa Usharika wa Mwenge (ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya hiyo) mchungaji Kaanasia Msangi akiimba kwa furaha siku hiyo

 Wanakwaya wa kwaya kuu ya Mwenge wakiwa jukwaani wakiimba kwa ustadi mkubwa.
Mwalimu wa kwaya ya Usharika wa Mwenge (ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya Vijana ) Mwalimu Kayese, akipata chakula cha mchana siku hiyo kabla ya kuanza kumwimbia Bwana wimbo  mpya

No comments:

Leave a Reply