Latest News


More

OMBENI KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO

Posted by : Unknown on : Saturday, May 11, 2013 0 comments
Unknown


OMBENI KATIKA JINA LA BWANA YESU KRISTO

MAOMBI NI NINI?

Maombi ni hali ya mwanadamu kuwa na mawasiliano na Mungu
Maombi kwa mwamini ni ibada tosha bila kujali anafanya hayo maombi wapi na kwa muda gani
Maombi ni tendo la imani kwa mwamini
Maombi ni njia ambayo mwamini anaitumia kuvumbua vitu ambavyo havionekani; katika ulimwengu wa giza
Maombi ni hali ya mwamini kumtegemea Mungu
Maombi ni maisha ya mwamini
Muda wa maombi ni muda wa kuwekeza , ni kipindi cha kupanda
Mfano Yesu Kristo alitumia muda wake mwingi na wa kutosha kuomba

“Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko"….Marko 1:35

Pia waweza kusoma Luka 6: 12 na Luka 22: 40 – 45
Maisha ya maombi hubadilisha sura ya nje ya mtu
Mungu anajibu maombi;ndio maana alituagiza tuombe (Mathayo 7:7-11)
Ø  Maombi ni silaha kubwa sana kwa mwamini;kuomba kunaleta mafanikio makubwa sana kwa waaminio
Ø  Mungu anasemaje  kuhusu maombi ? Yohana 16:24;

“Hata sasa hamkuomba neon kwa jina langu;ombeni nanyi mtapata,furaha yangu iwe timilifu”

Hii ina maana kwamba Mungu furaha yake ni kujibu maombi yetu, ila hatujibiwi kwa sababu hatuombi vizuri, twaomba kwa faida yetu wenyewe
Mungu anajibu maombi hivyo kwa mwamini isipite siku bila ya kuomba
Kumbuka maombi ya Ibrahim yalimwokoa Nduguye Lutu pale ambapo Mungu alivyotaka kuiangamiza Sodoma na Gomora

Lakini;
Kuomba kunaambatana na kusoma neno la Mungu wakati wote
Maombi ni maisha ya mwamini ya kila siku (Zaburi 55: 16 – 17)
Maombi hayana saa, siku au siku maalum, ila Mungu anasikia maombi yetu saa, na wakati wowote tumwombapo  1 Yohana 5: 14-15)

KUMBUKA;
Maombi huumba hivyo tusiombe maombi mabaya
Usimwombee mtu mabaya kwa kua amekufanyia jambo baya.Mwombee mambo mazuri siku zote
Maombi mabaya majibu yake yanatoka na kujibiwa toka katika ufalme wa giza (kwa shetani) na wala sio kwa Mungu
Mungu anasema mwombee adui yako mema na wala sio mabaya
Wengine wanaomba maombi ya kichawi, mfano baba mdhoofishe kabisa yule adui yangu, mtupe kuzimu…hayo ni maombi ya kichawi.Kama mwamini wa kweli huwezi kuomba maombi kama hayo

VIZUIZI VYA MAOMBI
1.       Mtazamo mbaya wa mwombaji
Mtazamo mbaya ni sumu ya maombi ya mwamini kujibiwa
Uwe positive katika maombi yako

2.       Hofu huzuia maombi
2 Tim 1 – 7
·         Mtu anayesita sita katika njia yake hawezi kupokea toba kwa bwana
·         Jinsi Mungu alivyo ndivyo nasi tulivyo kuwa Positive katika kile tuombacho
·         Imani na hofu ni maadui wawili ambao hawakai pamoja hata siku moja
·         Tafsiri ya hofu siku zote ni kumwambia Mungu hawezi kujibu maombi yako
·         Ukimtegemea Mungu hofu yote hupotea
·         Mtu mwenye hofu maombi yake hayajibiwi  (Yakobo 1: 5 – 7)

3.       Uasi (dhambi)
Aina yoyote ya kutomtii Mungu ni dhambi
Dhambi ni matokeo ya kuasi au kutokutii
Yakobo 1: 21 -22, Isaya 59:1 – 3, Mithali 28: 9 na Zab 66: 18 – 29

4.       Mahusiano mabaya ya kifamilia
1 Petro 3:7
“Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, na kumpa mke heshima , kama chombo kisicho na nguvu;na kama warithi pamoja wa neema ya uzima,kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe"

5.       Uchungu na kutokusamehe
Hiki nacho ni kikwazo cha mwamini kutokujibiwa maombi yetu.Unapokosewa na mtu basi samehe ili na wewe usamehewe na Mungu

NAWATAKIA WEEK END NJEMA!!

Mungu awabariki sana!

Kichila Tumaini S

No comments:

Leave a Reply