Latest News


More

USHARIKA WA KARIAKOO KUJENGA KITUO KIKUBWA CHA MAOMBI BAGAMOYO

Posted by : Unknown on : Thursday, July 18, 2013 0 comments
Unknown
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Kariakoo mchungaji Eliona Kimaro

 Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Kariakoo uko katika ujenzi wa kituo  kikubwa na cha kimataifa cha maombi huko Bagamoyo.Kituo hicho ambacho kiliwekwa jiwe la msingi tarehe 14/07/2013 na mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dr Alex Malasusa na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye alikua ni Makamu wa Rais wa Tanzania Mheshimiwa Dr Mohamed Gharib Bila na wageni wengine wengi wa ndani na nje ya Tanzania

Kituo hicho kitakua na sehemu ya kuabudia, sehemu kubwa ya maombi, viwanja vya michezo, hostel na hotel kubwa na ya kisasa

 Picha ya kanisa linalotarajiwa kujengwa kwenye kituo hicho cha kimataifa huko Bagamoyo
 Sehemu ya majengo yanayotarajiwa kujengwa

Mgahawa mkubwa na wa kisasa utakavyoonekana mara baada ya kumalizika
 Eneo lote jinsi litakavyoonekana mara baada ya kukamilika
 Ujenzi unavyoendelea kwa kasi mpaka sasa hivi


 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo hicho cha kimataifa
Blog hii inawatakia kila la heri katika maono hayo ya watu wa Mungu

No comments:

Leave a Reply