Latest News


More

MATUMIZI YA ULIMI...UNAUTUMIAJE ULIMI WAKO?

Posted by : Unknown on : Sunday, August 18, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
Matumizi ya Ulimi


Mchungaji Kaanasia Msangi (pichani juu) akihubiri katika ibada jumapili hii katika kanis ala K.K.K.T Usharika wa Mwenge alisema Yesu Kristo aliwaasa wanafunzi wake wajilinde na choyo za Mafarisayo.

Akinukuu somo la injili kutoka Luka 12:13-21 alisema mtu mmoja alimwambia Yesu Kristo ;mwalimu mwambie ndugu yangu anigawie urithi wangu..Alimwambia Yesu akijua kwamba anaweza kufanya jambo lolote na hata kumlazimisha nduguye amlipe au ampe urithi wake

Hii ni baada ya kuona ndugu yake anataka kumdhulumu sehemu ya urithi wake, na alijua ni Yesu pekee anaueweza kumsaidia.

Hapa tunajifunza kwamba watu wengi wamekua wabinafsi na wasio na upendo.Kama ukimpenda ndugu au rafiki yako huwezi kumwaibisha au kumdhalilisha mbele ya watu wengi kama alivyofanya ndugu huyu

Lakini Yesu alimwambia kila jambo lina majira na wakati wake

Yesu alimwambia nani aliye niweka kuwa msimamizi na mwamuzi wa mali yenu?.Yesu alionyesha ufalme wake si ufalme wa dunia hii wa kutawala na kugawa urithi

Yesu anasema katika Luka: 12:31 “Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa”

Yesu anatoa angalizo akisema jilindeni na choyo

Mara nyingi mtu anapokua na utajiri ana weza kufikia mahali akamsahau Mungu wake.

Utajiri si dhambi , alisema mchungaji Kaanasia Msani.

Tatizo ni jinsi ya kuutumia utajiri ulio nao

Mambo ambayo yalimfanya tajiri kuonekana mpumbavu

Mchungaji Msangi alisema kuna mambo sita ambayo yalimfanya tajiri kuonekana mpumbavu kama ifuatavyo;

1. Hali ya kushindwa kutambua alipopata utajiri wake umetoka wapi…Kumb 8:11

Hakukumbuka kutoa fungu la kumi,kutoa sadaka kwa Mungu,Malimbuko nk

2. Anashindwa kutambua nini cha kufanya na mali yake

3. Anafanya mali kuwa ulinzi wake badala ya Kumweka Mungu mlinzi wake…Zab 103:1-2;1Tim 6:17-19

4. Anapanga kutumia mali zake baadaye.Akijihakikishia ya kwamba ana uhakika wa kuishi miaka mingi.Ana upendeleo wake mwenyewe

5. Nje ya ufalme wa Mungu , nje na mapenzi na makusudi ya Mungu..Yakobo 4:13-14.Hatujui la kesho

6. Alitafsiri vibaya maana ya maisha.Mungu anasemaje kuhusu maisha?

Anasema maisha ni zaidi ya kula na kunywa.Maisha yetu yawe ni ya kuutafuta ufalme wa Mungu kwanza;na mengine Mungu atakuzidishia

Mwisho mchungaji Msangi alisema ulimi unaweza kuutumia vizuri kwa utukufu wa Mungu

Ibada hiyo ilikua maalum kwa kusifu na kuabudu na iliongozwa na mwinjilisti Mwigune na mhubiri Mchungaji Kaanasia Msangi
Kwaya zilizohudumu ni pamoja na kwaya kuu ya Ushaeika wa Mwenge, kwaya ya vijana, kwaya ya uinjilisti , kwaya ya akina mama na kwaya ya kusifu na kuabudu ya ushharika wa Mwenge

 Waimbaji wa kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge wakiimba kwenye ibada hiyo ya jumapili
 Washarika wakiimba na kusifu kwenye ibada hiyo
 Washarika wa Usharika wa Mwenge wakiimba na kusifu kwenye ibada hiyo maalum ya kusifu na kuabudu











No comments:

Leave a Reply