Latest News


More

FAMILIA YA NATAI YAOMBOLEZA KIFO CHA NDUGU YAO

Posted by : Unknown on : Wednesday, September 4, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :




Familia ya Natai leo imeomboleza na kuaga mwili wa dada yao  Eunice Elias Natai aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita
Marehemu alipatwa na mauti hiyo katika hospitali ya Massana Mbezi Beach alikokua amelazwa kwa muda mrefu.Ibada ya kuaga mwili wa marehemu imefanyika leo katika Usharika wa K.K.K.T Mwenge na kuongozwa na mwinjilisti wa Usharika wa Msewe ambako marehemu alikua anasali hadi mauti ilipomfika
Marehemu alizaliwa tarehe 15/11/1967 na kufariki tarehe 01/09/2013, na ameacha mtoto mmoja wa kiume.Mwili wa marehemu umesafirishwa leo  mchana kuelekea Moshi sehemu za Lukani, Bomang'ombe kwa mazishi


 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo



 Mwinjilisti wa Usharika wa Msewe akihubiri katika ibada hiyo.Marehemu alikua msharika wa Msewe

 Msemaji wa familia akisoma wasifu wa marehemu


Bwana Mushi mwanachama wa WANAWAMA akitoa rambirambi zake kwenye ibada hiyo.


 Mtoto wa marehemu akilia kwa uchungu kwenye ibada hiyo.Pembeni yake ni Mzee Godlisten Lema akimfariji
 Wana familia wakiandaa mwili wa marehemu tayari kwa kutoa heshima zao za mwisho
 Baadhi ya ndugu na marafiki wakitoa heshima zao za mwisho

 Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu kwenye ibada hiyo


 Mtoto wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa marehemu mama yake
 Dada wa marehemu akilia kwa uchungu wakati akitoa heshima za mwisho

 Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari tayari kwa safari yake ya mwisho ya maziko huko Moshi





Mwinjilisti wa Usharika wa Msewe akitoa neno la mwisho kwa ndugu na marafiki wanaosafiri kuelekea Moshi kwa mazishi
"MWENYEZI MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI .AMEN"

No comments:

Leave a Reply