Latest News


More

HARUSI YA ISAYA MHEMA ILIVYOPENDEZA

Posted by : Unknown on : Thursday, November 14, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,
 Isaya Mhema jumapili ya tarehe 22/09/2013 alifunga ndoa na Christina Lucas.Ndoa hiyo ilifungwa katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge na kuhudhuriwa na ndugu jamaa na marafiki toka sehemu mbalimbali
Baadaye ilifanyika tafrija ya nguvu katika ukumbi wa TBS Ubungo.

 Maharusi wakiingia ibadani tayari kuanza ibada hiyo
 Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge akiwapokea bwana harusi na mpambe wake tayari kuanza ibada hiyo ya ndoa
 Mzazi akimwingiza bibi harusi kwenye ibada tayari kufanya ibada ya ndoa
 Maharusi wakiwa kwenye ibada hiyo
 Kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge ikiimba kwenye ibada.Kwaya hii pia mara nyingine bwana harusi huimba haswa kwenye matukio makubwa ya kanisa
 Kwaya ya vijana ya Usharika wa Mwenge ikiimba kwenye ibada hiyo.Bwana harusi naye ni mwimbaji wa kwaya hii
 Kwaya ya Vijana ya Usharika wa Ubungo wakiimba kwenye ibada hiyo.Bi harusi ni mwimbaji wa kwaya hii
 Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge

 Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi  akichanganya soda kama alama ya ushirika wa bwana harusi na bi harusi.Mchungaji Kaanasia Msangi alisema ukichanganya soda ya fanta na coca cola huwezi kuitenganisha.Vivyo hivyo kwa ndoa ya bwana na Bi Mhema haiwezi kutenganishwa

 Maharusi wakivishana pete kwa furaha kubwa
 Bwana harusi Isaya akiweka saini kwenye  cheti cha ndoa
 Bi harusi bi Christina akiweka saini cheti cha ndoa

 Bwana harusi akiimba na kwaya yake ya Vijana ya Usharika wa Mwenge.
Kulikua na kwaya sita zilizohudumu kwenye ibada hiyo.Kwaya ya akina mama wa Usharika wa Mwenge, kwaya ya Vijana ya Usharika wa Mwenge,Kwaya ya Vijana ya Usharika wa Ubungo, kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge, Kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Mwenge, na kwaya ya watoto ya Usharika wa Mwenge
 Maharusi  wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa
 Maharusi wakiwa na wazazi wao.Mpambe wa bwana harusi ni bwana Huruma Mgata na Matron ni Rachel Mgata ambaye ni mke wa Huruma
 Picha ya pamoja mbele ya kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge
 Baadaye ilifanyika tafrija ya nguvu katika ukumbi wa TBS Ubungo.Pichani juu ni keki iliyoandaliwa kwa ajili ya maharusi


 Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini TBS Ubungo
 Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akiwa na mumewe Bwana Msangi.Pembeni ni bwana Shujaa
 Maharusi wakitambulishwa ukumbini
 Maharusi wakikata keki
 Maharusi wakilishana keki
 Mzazi wa bi harusi akitoa utambulisho

 Picha ya pamoja na familia
 Katibu wa baraza la wazee wa  Usharika wa Mwenge Mzee Kombe, watatu kutoka kwa mzee Kombe ni wazee wa kanisa wa Usharika wa Mwenge Dr Lilian Kitunga na wa mwisho ni mzee mama Laita Ngole
 Bwana harusi wakifanya utambulisho siku hiyo
 Parish worker wa Usharika wa Mwenge Suzan Mwimbe akitambulishwa
 Maharusi wakipakua chakula
Maharusi wakilishana chakula
Bwana harusi ni mwenyeji wa Njombe, kabila ni Mbena na bi harusi ni mwenyeji wa Tabora, kabila ni Mnyamwezi
Mtandao huu unawatakia kila la kheri na baraka tele katika ndoa yao hii!!
(Samahani sana picha hizi zilichelewa kutufikia)

No comments:

Leave a Reply