Latest News


More

UMUHIMU WA KUWEKA NADHIRI NA KUITOA

Posted by : Unknown on : Sunday, March 23, 2014 0 comments
Unknown


UMUHIMU WA KUWEKA NADHIRI NI KUIONDOA KWA WAKATI


Neo Kuu 1 Samwel 1 :10-11
Neno la waraka Kol 1:16-17
Zaburi 123

Umuhimu wa kuweka nadhiri kwaMungu ni kiiondoa kwa wakati.Akihubiri katika  ibada ya jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mchungaji Mchomvu  amesemanadhiri ni ahadi ambayo mtu anaweza kutoa
Akitoa mfano katika kitabu cha 1 Samwel1_10-11 amesema Anna alikua mke wamkubwa wa Elikana na mke mdogo aliitwa Penina
Hannah hakujaliwa kupata motto ila Penina alikua na watoto.Elikana aliwapenda wake zake wote ila alimpenda Penina zaidi kwa kua alikua na watoto
Hawa wake wawili hawakua wakipatana kwa kua Penina alimchukia zaidi Hannah kwa kukosa watoto.Mara nyingi alikua anamchokoza na kumuudhi Penina hata wakati wakienda ibadani.Lakini Hannah aliendelea kuwa magotini kwa Mungu na kuomba kwa bidii na akaweka nadhiri kwa bwana akiomba kwa machozi na kulia na akasema kama bwana atamjalia kupata motto basi nadhiri yake kwa bwana ni kumtoa huyo motto amtumikie Bwana
Hannah alitoa ahadi yake hii toka rohoni
Biblia inasema ili nadhiri iwe na maana ni lazima ukumbuke kuitoa kwa wakati au kuitimiza kwa wakati
Mungu hupendezwa sana na watu wanaoweka nadhiri na huwa hakawii kuitimiza kwa Yule aliyeiweka alisema mchungaji Mchomvu
Mungu aliitimiza nadhiri ya Hannah na Hannah naye alitimiza nadhiri yake kwa bwana kwa kumtoa motto wake Samwel amtumikie bwana
Inawezekana unaweka nadhiri lakini je; ina tija kwa bwana? Je unaweka nadhiri kwa mahitaji yako binafsi au kwa manufaa ya Mungu na wanadamu
Mungu anapenda yeye awekae nadhiri ambayo ina tija kwa bwana na wanadamu pia
Ondoa nadhiri yako mapema mara tu baada ya kuipata
Tafakari nadhiri yako uliyoiweka kwa bwana, je ulikwishaitoa? Kama bado hujachelewa itoe sasa
Upendo wa Mungu utadhihirika kwako pale tu utakapotoa na kuitimiza nadhiri kwa bwana alihitimisha mchungaji MchomvuIbada hiyo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi
  

Watoto wa shule ya jumapili wa Usharika wa Mwenge wakiwa katika ibada ya jumapili
Mwaliku wa shule ya jumapili Eliajua Geofrey  (pichani juu) akiongoza ibada hiyo ya leo

Wakristo wa Usharika wa Mwenge jumapili ya leo wameshiriki chakula cha bwana katika ibada zote tatu zinazofanyika katika ibada za kila jumapili
Pichani juu na chini washarika wakishiriki chakula cha bwana

No comments:

Leave a Reply