Latest News


More

KWAYA YA VIJANA KIMARA YAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA UIMBAJI NGAZI YA DAYOSISI

Posted by : Unknown on : Saturday, August 16, 2014 0 comments
Unknown
 
Mashindano ya Uimbaji wa Vijana ngazi ya Dayosisi yamefanyika leo katika Usharika wa Mbezi Beach wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  na kushirikisha kwaya za Vijana takriban toka sharika kumi na mbili za Dayosisi hii ya Mashariki na Pwani

Katika mashindano hayo kwaya ya vijana ya Usharika wa Kimara (pichani juu) imeibuka kidedea kwa kuchukua nafasi ya kwanza.Kwaya nyingine na nafasi zao ni kamaifuatavyo
2.Nafasi ya pili imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika wa Ubongo

3. Nafasi ya tatu imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika wa Kijitonyama

4.Nafasi ya nne imechukuliwa na kwaya ya Vijana ya Usharika wa Keko

5.Nafasi ya tano imekwenda kwa kwaya ya Vijana ya Usharika wa Mwenge

Washindi wa pili kwaya ya Vijana ya Ubungo wakiimba jukwaani leo




Pichani juuna chini ni waimbaji wa kwaya ya Vijana ya Usharika wa Mwenge wakiimba jukwaani...Walishika nafasi ya tano


 

No comments:

Leave a Reply