Washarika na watu mbalimbali wamejumuika jana katika maadhimisho ya miaka hamsini tangu kuunganika kwa makanisa saba ya Kilutheri nchini na kuunda Kanisa moja la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Kilele cha maadhimisho hayo yaliyoanza juzi yameadhimishwa katika Dayosisi ya Kaskazini, usharika wa Chuo Kikuu cha Tumaini (TUMA - Tumaini University of Makumira), Makumira, Usa River, Arusha yakiongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa.
KKKT inatokana na makanisa yaliyoanza kutekeleza utume wa kueneza Injili zaidi ya miaka 100 iliyopita nchini Tanzania. Mnamo tarehe 19 Jini 1963, makanisa yaliamua kuweka mbali tofauti zao na kuunganika na kuunda Sinodi na baadaye Dayosisi. Hadi Mei 26, mwaka huu, KKKT imefanikiwa kuwa na Dayosisi 22 na Misioni 20 zinazotoa huduma mbalimbali za kiroho kwa washarika wake na huduma za kijamii kwa wote kama vile mashule, vyuo vya mafunzo ya ufundi, Vyuo vya Elimu ya Juu, mabenki, mahoteli, mahospitali
Mwalimu Randy Stubbs toka Marekani ambaye pia ni mkufunzi wa Muziki chuo kkikuu cha Tumaini Makumira akiongoza upigaji wa nyimbo siku hiyo ya kilele
Maaskofu mbalimbali wakiongoza maandamano siku ya kilele cha miaka 50
Mkuu KKKT Mstaafu Askofu Dr.Samson Mushemba
Yeye yu hai mpaka sasa na kwa heshima na kumtahini ndiye aliyehubiri kwa siku ya jana yaani katika kilele cha maadhimisho ya Jubilii ya miaka 50 ya KKKT.
Katika mahubiri hayo mkazo wake mkubwa ulikuwa ni kulitaka "Kanisa kuwa na Umoja" Yohana 17:21 Hebu tudumishe umoja wetu kama Baba alivyo na umoja nasi na tuendelee kutimiza malengo ya Bwana Yesu Kristo" pamoja na kutimiza malengo yakuliunganisha Kanisa hili na kuwa KKKT.
Viongozi wakuu walioiongoza KKKT hadi sasa ni:
Askofu Stefano Ruben Moshi (1963 - 1976)
Askofu Dk Sebastian Kolowa (1976 - 1992)
Askofu Dk.Samson Mushemba (1992 - 2007)
Askofu Dk. Alex Gehaz Malasusa ( 2007 hadi sasa)
Maaskofu Dk Sebastian Kolowa na Stephano Moshi ni marehemu (Picha kwa hisani ya Sadataley.blog)
No comments: