Mwanaume mmoja kutoka Ujerumani anayeshikilia rekodi ya dunia
ya kuwa mtu aliyetoboa zaidi mwili wake, Rolf Buchholz amekatazwa kuingia
Dubai.
Rolf Buchholz, ametoboa mwili wake mara 453 ikiwemo usoni mwake na ana pembe
mbili juu ya paja la uso wake.Bwana Buchholz alieleza BBC kuwa maafisa wakuu katika uwanja wa ndege walihofia huenda alikuwa ni '' mchawi'' .
Mtaalamu huyu wa tarakilishi alitambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness, kama mwanaume aliyetoboa mwili wake zaidi duniani mwaka wa 2012.
Onyesho lake katika mgahawa maarufu wa Irque le Soir ulioko katika hoteli ya Fairmont Hotel Dubai lilifutiliwa mbali.
Bwana Rolf amesema kuwa mizigo yake bado iko Dubai na aliapa kwenye mtandao wa kijamii kuwa hatarudi tena katika milki za Kiarabu.
Polisi na Maafisa wa usafiri wa ndege nchini Dubai hawajazungumzia swala hilo.
No comments: