wa Globu ya Jamii
Askofu Beatus Kinyaiya |
Baba Askofu Beatus Kinyaiya alizaliwa Mei 9, 1957. Akapata daraja takatifu la Upadre katika shirika la Kimisionari la Wafranciscan Minor tarehe 25 juni, 1989.
Aliteuliwa kuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Mbulu tarehe 22 Aprili, 2006, na kusimikwa/ kuwekwa wakfu rasmi na Kardinali Polycarp Pengo kuwa Askofu wa jimbo la Mbulu Julai 2, 2006.
Na leo tarehe Novemba 6, 2014 ameteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dodoma ambalo nalo limepandishwa hadhi na kuwa Jimbo Kuu.
Askofu Beatus Kinyaiya atasimikwa rasmi kuanza utume wake huo mpya katika jimbo hilo mwezi wa Januari, 2015.
No comments: