Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibunu na kutolewa kwenye mtandao wa Dailyu Mail,robo tatu ya wanawake wenye mimba wanaamini kwamba wamekuwa wakiziweka rehani kazi zao kutokana na likizo hizo ndefu za uzazi.
Wanawake saba kati ya 10 waliohijiwa wameonyesha kwamba wamekuwa wakiingiwa na mashaka ya kuwekwa kando kazini na wamekuwa wakiziona kazi zao kuwa kitu cha thamani kuliko likizo wanazochukua baada ya kujifungua.
Utafiti huo uliofanywa kupitia mtandao wa maternitycover.com uliainisha kwamba kiwango cha juu cha woga kwa wanawake wanaopata ujauzito huhusiana zaidi na namna ya kuendelea kulinda ajira na taaluma zao.
Nusu ya wanawake 1,300 walioulizwa walieleza kwamba wanaona ni vyema kuficha ujauzito kwa kutowaeleza wakuu wao wa kazi hasa iwapo kuna nafasi ya kupata kazi mpya au kupandishwa daraja.
Sheria katika mataifa mengi zinaeleza kwamba wanawake wanatakiwa kupewa wiki 26 (miezi sita) kama kiwango cha kawaida kwa ajili ya likizo ya uzazi kwa kuwa nje ya kazi zao kisha kurejea.
Hata hivyo utafiti unaonyesha kwamba katika hali ya saa ya uchumi wa ushindani, nusu ya wanawake wanaona kwamba wanaweka rehani kazi zao kwa kuwa nje ya kazi kwa muda mrefu kwa ajili ya kuwa na watoto wao.
Watatu katika kila wananwake wanne wanaofanya kazi walisema ndoto za kupandishwa daraja hutoweka hasa wanapopata mimba na kujifungua na mmoja katika kila watatu wanaamini kwamba kipindi hicho hutoa fursa kwa wenzao kupandishwa madaraja badala yao.
(Source: Mwananchi)
No comments: