Latest News


More

Tanzania nzima sasa mambo ni kikombe

Posted by : Unknown on : Thursday, March 31, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,

Leo ni takribani siku kumi na moja tangu Dada Mange (maarufu kama bibi) aanze kutibu kwa kikombe kwa tiba anayodai kuwa kapewa kwa uwezo wa Mungu

Mtaa anaoishi wa Urban Quarter umeanza kuwa maarufu kama Loliondo kwa babu.Hadi jana watu takriban 2000 hivi walikua kwenye foleni kwa bibi tofauti na siku mbili zilizopita wakati walikuwepo watu 500

Kwa watanzania hii ni changamoto ambayo inabidi watu waamke na kuwa makini kwani kwa jinsi tunavyoendelea wataibuka watu wengi sana watakaodai wameoteshwa kutibu dawa.Swaali la kujiuliza ni hili je, hawa watu walikua wapi hawakujitangaza kabla ya babu wa Loliondo? Kwa kusema hivi sina maana kuwa ya babu ndio sahihi la hasha.Uhalali na ukweli wa dawa anaujua mgonjwa kwa imani yake, ila huu uibukaji wa wanaotibu dawa kwangu mimi ndio unanitisha na watu kama kawaida wanaenda kwa uwingi kupata dawa.

Kesho usishangae akaibuka mwingine Singida, Mwanza, Kigoma au mkoa mwingine ule.

Kazi kwetu watanzania


Pichani dada Mage (katikati) akiwa na mwandishi wa habari hii (keronyingi.blogspot) pamoja na ndugu wa bibi nyumbani kwao Tabora Dada kapandisha mashetani kabla ya kupewa kikombe kwa bibi
Mzuka umetulia baada ya kuombewa na kupata kikombe
Wana usalama nao hawako nyuma kuhakikisha mambo yanakua shwari kwa bibi
Foleni ndeefu kwenda kupata kikombe.Watoto, wakina mama na akina baba, wote wanaelekea kupata kikombe
Foleni inazidi kuwa kubwa
Gari la kamanda Barlow wa Tabora likiwa njiani kwenda kwa dada kuangalia usalama

Mkuu wa mkoa Abeid Mwinyimsa akiwa nyumbani kwa dada

Mkuu wa mkoa wa Tabora akisikiliza maelezo ya tiba kwa umakini
Kutoka kushoto ni RPC Barlow, mkuu wa mkoa Mwinyimsa na afisa usalama wa wilaya ya Tabora mjini
Afisa mwandamizi wa jeshi la polisi akiombewa kabla ya kupata kikombe cha dada