Latest News


More

Tusiwanyanyapae watoto wetu

Posted by : Unknown on : Monday, March 28, 2011 0 comments
Unknown
Mtoto Lu Hao wa nchini China

Juu na chini Mtoto Evelyn wa Mwenge Tanzania


Natamani kuwa kama mtoto.....

Aliimba Lady Jay Dee wimbo huu , natamani kuwa kama mtoto.

Mtoto mdogo huwa hajui kukasirika, hajui kuchukia na hata ukimchapa baada ya muda bado atakuja kwako na kukumbatia au hata kutaka umbebe...Huyo ndio mtoto alivyo..

Pamoja na hayo yote watu wazima, saa nyingine hata wazazi wamekua wanawanyanyasa sana watoto inafikia hata kuwapa vilema vya maisha kwa kuwachoma na moto au hata vitu vyenye ncha kali

Huu ni ukatili mkubwa sana haswa kwa mtoto ambaye hajui hawezi kukujibu au saa nyingine hata kukushtaki, hajui kukasirika au kuweka kinyongo moyoni

Wazazi, walezi na watu wazima tuache kunyanyasa watoto wadogo kama hawa

Huo ndio ujumbe wangu wiki hii

Nawatakia wiki njema na baraka tele kwa kila unalolifanya