Ilikua ni siku ya furaha nderemo na chereko kwa Cuthbert Noah na Matilda Elias pale walipoamua kufunga pingu za maisha.
Cuthbert ambaye ni mwajiriwa katika kampuni ya Vodacom aliamua kuuaga ukapera na kufunga pingu za maisha katika kanisa la K.K.K.T Kinondoni Hananasif na Matilda Elias na baadaye tafrija iliyofanyika katika ukumbi wa Mamba Club ulioko Kinondoni.

Pichani ni Bwana na Bibi harusi wakiwa katika ufukwe wa hoteli ya Golden Tulip walikoenda kupiga picha mara baada ya kufunga pingu za maisha

Bwana harusi akifanya utambulisho wa ndugu katika ukumbi wa Mamba Club
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ambaye pia ni mjomba wa bwana harusi Ndg Kichila akiwakaribisha wageni ukumbini

Mc wa sherehe hiyo akisherehesha katika Ukumbi wa Mamba Club Kinondoni siku hiyo

Maharusi wakiwa na wapambe wao katika ufukwe wa Golden Tulip Hotel.Katikai aliyevaa shati jekundu ni meneja wa hoteli hiyo ndugu Neel

Maharusi wakiwa na Junior (Cuthbert)

Maharusi wakiwa kwenye pozi kwenye hoteli ya Golden Tulip
Bwana harusi, msimamizi wake na mdau wa blog hii ndugu Kichila

Bwana harusi akiwa kwenye pozi

Bwana na bibi harusi
Junior naye alikuwepo
Tunaomba radhi wadau baadhi ya picha sio nzuri sana kutokana na kigugumizi cha mpigaji