Latest News


More

Posted by : Unknown on : Saturday, September 3, 2011 0 comments
Unknown
MHESHIMIWA EDWARD LOWASA (WAZIRI MKUU MSTAAFU) ACHANGIA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA LA K.K.K.T USHARIKA WA MWENGE

Waziri mkuu mstaafu Mheshimiwa Edward Lowasa aliongoza harambee ya ujenzi wa kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mwishoni mwa wiki iliyopita na kusaidia kukusanya takriban shilingi milioni 60 zikiwa ni ahadi pamoja na taslimu

Katika harambee hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali iliongozwa na msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ys Mashariki na Pwani mchungaji George Fupe
Katika mahubiri yake mchungaji Fupe alihimiza wazazi kuwalea watoto katika njia inayompasa na kumpendeza Mungu kwani ndio wakristo wa kanisa wa miaka ijayo.

Alitoa mfano kuwa aliwahi kutembelea nchi moja ya Ulaya na kukuta waumini kanisani ni wazee tu vijana hawaendi kanisani, na hii ni kwa sababu wazazi hawakuwaandaa watoto wao kumfuata Mungu

Aliwaasa waumuni wa Mwenge kuwa bila kuwaongoza watoto na vijana katika kumjua Mungu kanisa na nyumba ya Mungu wanayoijenga itakosa waumini katika miaka ijayo

Katika ibada ya harambee hiyo mheshimiwa Lowasa alichangia taslimu shilingi milioni 30.7 yeye pamoja na marafiki zake

Pichani ni waimbaji wa kwaya ya The Winners toka Usharika wa Ubungo ambao waliimba katika ibada hiyo

Baadhi ya waumini wakiwa katika ibada hiyo ya harambee

Mkuu wa jimbo la kaskazini akiwa pamoja na msaidizi wa askofu mchungaji Fupe (katikati) pamoja na mchungazi kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Sigala


Baadhi ya waumini wakiwa ibadani




Mheshimiwa Lowasa akiwa katika misa ya harambee hiyo.








Tatizo la umeme nalo lilikuwepo lakini mafundi walirekebisha na kuwasha generator ambalo liliokoa jahazi


Mafundi wakirekebisha generator baada ya umeme kukatika



Kwaya ya Upendo ( ya wamasai) nayo ilikuwepo kuhamasisha ujenzi siku hiyo





Msaidizi wa Askofu mchungaji Fupe akitoa mahubiri katika ibada hiyo





Wanakwaya wa The Winners wakiimba ibadani


Waumini wakitoa sadaka ibadani




Waumini wakiendelea kutoa sadaka







Godbles Lema (Mzee wa kanisa ) akiongoza waumini kutoa sadaka

Mama Chacha (mzee wa kanisa) akigawa bahasha kwa ajili ya sadaka maalum siku hiyo



Kwaya ya Uinjilisti Usharika wa Mwenge wakiimba ibadani





Mwalimu Mushi wa kwaya ya Uinjilisti akiongoza waimbaji wake kuimba siku hiyo




Ramani ya kanisa la Mwenge litakavyoonekana baada ya kukamilika






Wanakwaya wa Ubungo wakirudi kukaa baada ya kuimba Mc wa harambee hiyo Manase Ndanshau akimshukuru Mheshimiwa Lowasa mara baada ya kutoa mchango wake





Msaidizi wa askofu akiwa na mgeni rasmi Mh.Lowasa na M mc wa siku hiyo ambayo walitoka Usharika wa Sinza na Kijitonyama





Waumini wakitoa ahadi zao mbele ya mgeni rasmi


Mwana blog hii Tumainui Kichila naye alikuwepo kutoa ahadi yake mbele ya mgeni rasmi









Mc akihamasisha waumini kutoa ahadi zao







Vitu mbalimbali vililetwa kwa ajili ya mnada kama vile mahindi, mafuta ya kupikia, mbuzi, kuku na picha mbalimbali






Mc akimshukuru mke wa Mheshimiwa Lowasa baada ya kununua kitu katika mnada huo


















Msaidizi wa askofu akiwashukuru ma Mc wa siku hiyo kwa kazi nzuri bara baada ya mnada kumalizika











Kwaya ua Upendo ya wamasai walitoa zawadi ya mgolole kwa mgeni rasmi






Mheshimiwa Lowasa mara baada ya kupewa zawadi ya shuka maaluma la kimasai na wanakwaya wa kwaya ya Kimasai




Bango maaluma la kuhamasisha harambee hiyo




Mheshimiwa Lowasa akishikana mikono na wachungaji mara baada ya mnada kuisha












Mgeni rasmi akiagana na waumini mara baada ya ibada ya harambee kuisha



Mheshimiwa Lowasa akiagana na waandishi wa habari













Baada ya ibada waumini wote walipata bites pamoja na soda hapo hapo kanisani.Pichani Godbles Lema (mzee wa kanisa) akigawa bites kwa waumini