Latest News


More

SEND OFF YA ANGELA REGIS YAFANA - UKUMBI WA MAWELA SINZA

Posted by : Unknown on : Thursday, June 7, 2012 0 comments
Unknown
Saved under : ,

Angela Regis aliaagwa rasmi (send off) katika ukumbi wa Mawella ulioko Sinza karibu na ukumbi wa Vatican City.
Sherehe hiyo ya Send off ilihudhuriwa na mamia ya ndugu, jamaa na marafiki hakika ilifana sana na iliendeshwa na mshereheshaji maarufu hapa jijini Dr Cheni.Fuatilia picha hapa chini
 Bi harusi akiwa katika pozi

 Bi harusi na mpambe wake.Hakika walipendeza sana
 Hapa wakiwa ndani ya ukumbi maarufu wa Mawela
 Wageni wakiserebuka katika mtindo wa Ringi.Mtindo huu ni maarufu kwa kabila la Wachaga na uzuri wake ni kwamba usalama wa mifuko ni mkubwa kwani mikono yote huwa juu ya mabega.Hongera Wachaga kwa kucheza huku usalama wa mifuko ukizingatiwa
Baadhi ya ndugu wakiserebuka ukumbini siku hiyo

 Keki ya ndafu nayo ilikuwepo
 Mama mzazi wa bi harusi (Mama Mushi) aliyesimama mbele akiwa na mama mlezi wa kiroho nyuma yake na dada wa bi harusi katikati na dada mwingine wa bi harusi Lilian Kichila akiwa kwenye pozi na picha ya pamoja


 Mwenyekiti wa kamati Bwana Kichila  akifungua rasmi sherehe hiyo
 Mwenyekiti wa kamati ambaye pia alikua floor manager ndugu Tumaini Kichila akiendelea kuwakaribisha wageni kwenye sherehe hiyo
 Keki ya unga nayio ilikuwepo katika sherehe hiyo
 Bi harusi akilishwa keki na mama yake kama ishara ya kumtakia kila la heri na baraka tele

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi naye kwa heshima alipewa keki kama shukrwani kwa kufanikisha sherehe hiyo.Pichani ni mwenyekiti akipokea keki na mke wake Lilian Kichila


 Bi harusi  akielekea alikokaa bwana harusi mtarajiwa tayari kumkaribishwa kwenye chakula


 Maharusi watarajiwa wakielekea kupata msosi kwa mbwembwe nyingi.HAKIKAWALIPENDEZA


 Maharusi wakiwa kwenye eneo la msosi
Bwana Harusi mtarajiwa bwana Benn akilishwa na mke wake mtarajiwa Bi Angelina


 Lilian Kichila akiteta jambo na mmojawapo wa waalikwa  bwana na bi Mzava katika sherehe hiyo
 Bwana James Mushi na mke wake wakiwa kwenye meza ya wawekezaji wazawa.
 Mtumishi wa Bwana Mwinjilisti Godlisten Lema na Bwana Gerald Kimaro wakiteta jambo ukumbini hapo. wawekezaji wakiteta jambo katika hafla hiyo
 Hii meza yote ilikaliwa na wawekezaji wazawa na wake zao.Hakika walipendeza.Yuko Mtumishi wa Bwana Mwinjilisti Godlisten  Lema (anayeongea) na mke wake, Bwana James Mushi na mke wake na bwana Gerald Kimaro na mke wake.Hakika ilikua siku ya furaha kwa watu wote waliohudhuria
 Wakati wa zawadi marafiki wakienda kutoa zawadi zao
 Wafanyakazi wenzake na bi harusi wakitoa zawadi zao
Wafanyakazi wenzake na bi harusi wakiwa kwenye picha ya pamoja
 Madada wa bi harusi wakiongozwa na Lilian Kichila wakielekea kutoa zwadi zao


Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Tumaini Kichila akisindikizwa na wanakamati wenzake
 Wafanyakazi wenzake na dada wa bi harusi Lilian Kichila wakimtunza kama shukrwani kwake na pongezi pia.
 Wafanyakazi wenzake na dada wa bi harusi Lilian Kichila wakimfuta machozi kama pongezi
 Wanakamati wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati wakienda kutoa zawadi yao.

 Utambulisho wa kamati na picha ya pamoja
 Mwenyekiti akizungumza machache na kueleza zawadi yao kama kamati
 Mwenyekiti akikabidhi risiti ya zawadi kwa bi harusi
 Zawadi kutoka kwa wakwe wa bi harusi
 Dada wa bi harusi akiwa kwenye picha ya pamojana bi harusi na mpambe wake


Bi harusi na mpambe wake wakiaga tayari kuelekea nyumbani kupumzika hii kuashiria kwamba sherehe imekwisha
Saved under : ,

No comments:

Leave a Reply