Dada Happyness alifariki siku ya ijumaa baada ya kuugua kwa muda mrefu.Ibada ya mazishi ilifanyika katika Usharika wa K.K.K.T Mwenge na kuongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa K.K.K.T Kinyerezi akishirikiana na mchungaji wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi
Pichani juu watoto wa marehemu wakiongoza wakati wa kuingiza mwili wa marehemu Happyness kanisani Mwenge tayari kwa ibada ya mazishi.Nyuma ni wanakwaya ya akina mama Usharika wa Kinyerezi wakibeba mwili wa marehemu tayari kuuingiza kanisani kwa ajili ya ibada.
Watoto wa marehemu Kutoka kulia, Jackson, Neema , Aneth na mtoto wa ndugu yake marehemu wakiwa katika ibada ya mazishi
Wanakwaya wa kwaya ya akina mama Usharika wa Kinyerezi wakiingiza jeneza la mwanakwaya mwenzao katika kanisa la Mwenge tayari kuanza ibadaWanafamilia wakiwa kanisani wenye majonzi makubwa kwa kuondokewa na ndugu yao Happyness
Mwili wa marehemu Happyness ukiwa kanisani tayari kwa ibada leo mchana
Mtoto wa marehemu Neema akilia kwa uchungu mara baada ya kutoa heshima za mwisho
Msemaje wa Familia (ambaye ni mjomba wa marehemu) akiwashukuru watu waliojumuika pamoja kumzika marehemu Happyness kwenye makaburi ya Sinza
No comments: