Safari yangu ya mkoa wa Iringa nilibahatika kwenda mpaka wilaya ya Mufindi mahali ambapo inaaminika ni makao makuu ya baridi hapa Tanzania
Japo miezi hii baridi haijaanza lakini kwetu sie tuliotoka mwambao wa Pwani ni baridi kali.Ukikutana na wenyeji wanakwambia baridi bado wakati sisi tulikua tumevaa makoti makubwa.Baridi haswa hua inaanza miezi ya nne katikati kwenda miezi ya saba wakati mwezi wa sita ndio miezi ya kilele cha baridi
Mazao makuu ya biashara katika wilaya hii ni pamoja na chai kama inavyoonekana ikiwa imestawi vizuri
Safari yangu nikielekea katika Kiwanda cha Mgololo ambacho kipo wilayani Mufindi.Nilikuta mlima ambao naweza kusema ni mkali kuliko ule mlima Kitonga unaopanda kabla ya kufika mjini Iringa.Huu ni mlima Mgololo
Picha ya juu ni mteremko wa mlima Mgololo.Hii barabara ni ya lami lakini ni kipande hiki tu cha mlima kimewekwa lami .Sehemu nyingine yote ya barabara toka Mafinga hadi Mgololo ni vumbi
Mlima huu ni mkali kiasi ya kwambba ukiangalia upande wa bondeni unaweza ukafunga macho kama ni mwoga hadi ufike chini ya mlima huo
Angalia kona ilivyo kali na upande wa kulia ulivyo
No comments: