Latest News


More

SIKU YA KUZALIWA MANDELA KUSHEREHEKEWA

Posted by : Unknown on : Wednesday, July 3, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ameambia taifa hilo lianze kujiandaa kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Mandela tarehe 18 mwezi Julai.


Mandela ambaye anaheshimika sana kote duniani, atafikisha umri wa miaka 95,lakini kwa sasa angali mahututi hospitalini mjini Pretoria.

Alilazwa hospitalini tarehe 8 mwezi Juni akiwa na maradhi ya mapafu.

Kauli ya Zuma inakuja baada ya mke wa zamani wa Mandela Winnie Mandela, kukashifu chama ha ANC kwa kumnasa kwa video Mandela, walipomtembelea kwake nyumbani mwezi Aprili.

Kanda hiyo ilionyesha Mandela akiwa na mshangao na bila ya tabasamu wakati wa ziara ya mmoja wa vigogo wa ANC nyumbani kwake.

Winnie Madikizela-Mandela, alisema "kweli siwezi kueleza ambavyo familia ilihisi uchungu kuhusiana na kanda hiyo, na haikupaswa kwa jambo hilo kufanyika.''

Ikijibu tuhuma hizo, chama cha ANC kilitetea ziara hiyo, kikisema kuwa haikuwa na njama ya kutaka kujitafutia umaarufu.
Hapo Jumatatu, rais alitoa taarifa kusema kuwa wananchi wa Afrika Kusini waanze kujiandaa kwa sherehe za kuzaliwa kwa Madiba.

"lazima sote tufanye angalau jambo zuri kwa sababu ya utu kwa siku hiyo kama ujumbe wetu mzuri kwa Mandela,'' alisema Zuma.

Mandela anasifiwa sana kwa kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, nchini Afrika Kusini na kisha kuhubiri maridhiano licha ya kufungwa jela kwa miaka

27.

Alituzwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993 na kisha kuchaguliwa kama rais mwaka uliofuata. Aliondoka mamlakani mwaka 1999 baada ya kutawala kwa muhula mmoja.

No comments:

Leave a Reply