Katika huduma ya Yesu hapa duniani hakuwabagua watu kwa jinsia, rika au hali waliokua nayo.
Akifundisha katika ibada ya jumapili katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mchungaji Erasto Shaila (pichani juu) alisema Yesu Kristo alikuja kuhudumia na kuponya watu wote wenye uhitaji na aliweza kuponya hata wagonjwa
Katika somo la Luka 4:38-44 linaonyesha Yesu Kristo akihudumia watu wenye uhitaji na Yesu aliweza kukemea mama aliekuwa mgonjwa naye akapata uponyaji
Watu wengi waliwaleta wagonjwa wao nao wakapata uponyaji kabisa.Hakuna aliyerudi pasi na kuponywa au kupata uponyaji.
Watu walimtaka Yesu Kristo abaki nao asiondoke
Ubaguzi siku zote unasababishwa na upendeleo na ubinafsi alisisitiza mchungaji Shaila
Yesu Kristo anasema injili lazima ihubiriwe kwa kila kiumbe na kila taifa pasipo kubagua yoyoye yule
Ibada hiyo iliyokuwa na tendo la kushiriki sakramenti ya meza ya bwana na kupambwa na vikundi vya uimbaji kama vile kwaya kuu, kwaya ya uinjilisti,kwaya ya akina mama, kikundi cha praise and worship team na mwimbaji Joshua Mlelwa na mkewe
No comments: