Latest News


More

ASKOFU DR.MALASUSA KUONGOZA HARAMBEE KUBWA USHARIKA WA MWANANYAMALA

Posted by : Unknown on : Friday, July 5, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,


Kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwananyamala umeandaa ibada maalum ya harambee ya ununuzi wa nyumba ya mtumishi jumapili hii.

Akizungumza na mtandao huu Mchungaji kiongozi wa Usharika huo amesema yeye na ofisi yake wakishirikiana na baraza la wazee na washarika wa Mwananyamala kwa ujumla wanawakaribisha waumini mbalimbali kuhudhuria katika ibada hiyo maalum ya harambee ya ununuzi wa nyumba ya mtumishi

Ibada hiyo itafanyika tarehe 7/07/2013 mwaka huu katika Usharika wa Mwananyamala na kuongozwa na mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania  ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) Dr. alex Malasusa

Ibada hiyo itakuwa moja na itaanza saa mbili kamili asubuhi.Kwaya zitakazohudumu katika ibada hiyo ni kwaya zote za Usharika huo na kwaya kuu ya Usharika wa Mabibo External.

Neno kuu litakaloongoza: "Ndipo hao watu wakafurahi, kwa sababu wametoa kwa hiari yao wenyewe, kwa sababu kwa ukamilifu wa moyo kwa hiari yao wenyewe, wamemtolea Bwana;mfalme Daudi naye akafurahi kwa furaha kuu.
Daudi akamshukuru Mungu" 1Nyakati 29:9

Namba za kuchangia ununuzi wa nyumba hiyo ni;
 - Tigo Pesa 0712-135232
 - M - Pesa 0769-403619
K.K.K.T Mwananyamala akauni no: 001001032564270001  - AZANIA BANK

"MUNGU AWABARIKI"

No comments:

Leave a Reply