Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia leo tarehe 29/08/2013 katika hospital ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo cha askofu huyu maarufu zimetolewa na mtoto wake Mwiinjilisti Daniel Kulola ambaye ameitoa kupitia mtandao wa face book ,ambapo ameueleza umma wa watanzania kuwa baba yake mzazi amefariki dunia katika hospitari ya Aga khani ambako alikuwa amelazwa.
Hajaeleza marehemu alikua anaumwa nini lakini taarifa zinasema amekuwa mgonjwa siku nyingi ambapo aliwahi kulazwa nje ya nchi na baadae akarudishwa nchini na hatimae kufariki Dunia.
Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa watoto 10 ambapo saba bado hai. Alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuan makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.
Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
"Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la lake lihimidiwe."
No comments: