Uzinduzi wa Dayosisi hiyo mpya ulienda sambamba na kumwingiza kazini Askofu wa kwanza wa Dayosisi hiyo Askofu Emmanuel Makala. Askofu Makala pichani juu akiwa na mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Dayosisi hiyo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr Gharib Bilal
Dayosisi hiyo ilizinduliwa ikiwa na waumini wapatao 49,476 katika sharika 34 na mitaa 113
Pia Dayosisi hiyo ina majimbo matano ambayo ni jimbo la Kusini Maganzo, jimbo la Magharibi Kahama, jimbo la Bariadi, jimbo la Shinyanga na jimbo la Mashariki Maswa
Mkuu wa kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania Askofu Dr Alex Gerhaz Malasusa akiweka wakfu kiti ambacho atatumia Askofu Emmanuel Makala.
Hiki ndio kiti atakachotumia kukalia Askofu Emmanuel Makala
Pichani Makamu wa Rais Dr Gharib Bilal akisoma risala katika ibada hiyoViongozi mbalimbali wa serikali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mkuu wa kanisa la K.K.K.T ambaye ndiye aliyeongoza ibada hiyo akitoa shukurani mara baada ya kumaliza kazi ya kumsimika Askofu Emmanuel Makala kama mkuu mpya wa Dayosisi hiyo
(Naomba radhi wasomaji wa blog hii taarifa hii ilichelewa kidogo kutufikia )
No comments: