Latest News


More

HIVI UNAWEZA KUMTAKIA MSAMAHA KONY?

Posted by : Unknown on : Wednesday, September 18, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
 
Mtawa anayesaidia waathiriwa wa kike waliotendewa unyama na kundi la waasi la LRA, katika Jaumuhuri ya kidemokrasia ya Congo, anatarajiwa kutuzwa na shirika la Umoja wa Mataifa kwa kazi yake nzuri.

Tangu mwaka 2003 mtawa huyo Angelique Namaika, amesaidia zaidi ya wanawake 2,000 na wasichana waliodhulumiwa na LRA na kupoteza makao yao kutokana na mapigano.

Atapokea tuzo hiyo mwishoni mwa mwezi na kisha baadaye atakutana na Papa Francis.

Aliambia BBC kuwa ameshtushwa sana na hatua ya kumteua kwa tuzo hilo na kuwa atamtaka Papa kumsamehe Joseph Kony.

Kony, ambaye ana wapiganaji kati ya 200 na 500 katika kundi lake anatakikana na mahakama ya ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita.

Ameendesha harakati zake za kivita nchini Uganda, Sudan Kusini , Kaskazini Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati kwa zaidi ya miongo miwili.

Wapiganaji wake wanajulikana kwa kuvamia maeneo ya vijijini na kuwasajili kwa nguvu watoto kama wanajeshi kumpigania na kuwafanya watumwa wa ngono.

Baadhi ya wanawake waathiriwa wa harakati za kundi la LRA



''Pia nitamuomba Papa aweze kuingilia kati hali ya vita ili amani iweze kupatikana,'' alisema Angelique

Tuzo la 'Nansen Refugee', hutolewa kila mwaka na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kuwatambua wanaofanya juhudi za kipekee kuwasaidia wakimbizi walio katika mazingira magumu.

Angelique alifungua kituo katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa mji wa Dungu katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambako UN inasema kuwa sio rahisi kupata maji safi na kwamba barabara ni duni sana.

Mtawa huyo aliambia BBC kuwa kitu muhimu kwake kwanza ni kuwasaidia wanawake na wasichana waliaochwa bila makao kuweza kujifunza lugha ya wenyeji, ili waweze kuwasiliana na wenye biashara reja reja na kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Angelique aliambia BBC kuwa huwafunza kushona, kupika na kuoka mikate au keki ili kuwasaidia kujikimu kimaisha.

No comments:

Leave a Reply