Latest News


More

Nani akomeshe mateso haya kwa wanawake ; Mke akatwa mkono na mpenziwe

Posted by : Unknown on : Wednesday, September 11, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
Kuna mikasa mbalimbali huwatokea watu katika suala zima la mapenzi, kiasi cha kusababisha baadhi yao kutopenda tena kuingia kwenye jambo hilo wakiliona kama ni kitu kisichofaa, ingawa ukweli unaweza kuwa sio huo.
“Sitaki tena wanaume, ni watu wabaya, wameniumiza moyo wangu mno,” anasema Hawa Francis, mkazi wa Ubungo, Dar es Salaam. Sababu kubwa ni kero ambazo amewahi kuzipata katika suala zima la uhusiano. Vivyo hivyo wapo wanaume hawataki kuoa, kwa maelezo kuwa kuna wanawake wamewahi kuwatesa.
Kama wewe ni kati ya watu ambao umekata tamaa na suala la uhusiano, fahamu kuwa si wewe pekee.Kuna kundi kubwa la watu wameshatendewa kiasi cha kufanya wasiwe na raha tena.
Mkasa wa mwanamke kukatwa mkono

Ilikuwa Agosti 7, mwaka huu, saa mbili usiku. Ilikuwa ni siku iliyobadili historia ya maisha yake. Baada ya kuwa katika mapenzi na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka 17, wakipendana na kuitana majina yote mazuri unayoyajua yakiwamo kuambiwa ‘mpenzi wangu nakupenda, nikinywa maji nakuona kwenye glasi’…leo mapenzi yamegeuka shubiri.
Mwanamke huyo, Mchali Kihiyo (35), mama wa watoto sita, aliyepoteza viungo vyake kutokana na ukatili wa kijinsia uliofanywa na mwanaume ambaye wamekuwa na uhusiano nae (jina limehifadhiwa).
“Uhusiano wetu ulikuwa mzuri, hata hivyo kwa sasa naona mambo yamekuwa magumu kwangu, leo hii mimi sina mkono wa kushoto na nimeondolewa sehemu ya viungo vyangu vya upande mmoja,”anasema Mchali,akibubujikwa machozi kutokana na ulemavu alioupata.

Chanzo cha ulemavu
Anasema maisha yao ya uhusiano yalikuwa ya furaha kwa kipindi chote lakini yamegeuka shubiri baada ya mwanamume wake huyo kuonyesha dalili ya kutompenda kama awali, hali ambayo anaitafsiri kama labda alikuwa na mwanamke mwingine.
Mchali, anasema mikasa na mateso ilianza miaka mitatu iliyopita baada ya kuhisi kwamba mwanamume wake huyo amezaa na mwanamke mwingine. Ubaya zaidi ulimtokea baada ya mtoto wa huyo mwanamke mwingine, kutumbukia kwenye kisima cha maji na kisha kupoteza maisha.
“Kifo cha mtoto huyo, ndicho kilichozaa tatizo hili la ukatili dhidi yangu na kunisababishia ulemavu, kwa kuwa huyo mwanaume wangu na huyo mwanamke aliyezaa nae, walidai kwamba mimi ndiyo nilimtupia majini marehemu mtoto wao ili afe,”anasema mama huyo.

Source:Mwananchi Communication!
Saved under :

No comments:

Leave a Reply