Baadaye ilifanyika tafrija ya nguvu katika ukumbi wa TBS Ubungo.
Maharusi wakiingia ibadani tayari kuanza ibada hiyo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge akiwapokea bwana harusi na mpambe wake tayari kuanza ibada hiyo ya ndoa
Mzazi akimwingiza bibi harusi kwenye ibada tayari kufanya ibada ya ndoa
Maharusi wakiwa kwenye ibada hiyo
Kwaya ya vijana ya Usharika wa Mwenge ikiimba kwenye ibada hiyo.Bwana harusi naye ni mwimbaji wa kwaya hii
Kwaya ya Vijana ya Usharika wa Ubungo wakiimba kwenye ibada hiyo.Bi harusi ni mwimbaji wa kwaya hii
Waumini wakiwa kwenye ibada hiyo katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akichanganya soda kama alama ya ushirika wa bwana harusi na bi harusi.Mchungaji Kaanasia Msangi alisema ukichanganya soda ya fanta na coca cola huwezi kuitenganisha.Vivyo hivyo kwa ndoa ya bwana na Bi Mhema haiwezi kutenganishwa
Maharusi wakivishana pete kwa furaha kubwa
Bwana harusi Isaya akiweka saini kwenye cheti cha ndoa
Bi harusi bi Christina akiweka saini cheti cha ndoa
Bwana harusi akiimba na kwaya yake ya Vijana ya Usharika wa Mwenge.
Kulikua na kwaya sita zilizohudumu kwenye ibada hiyo.Kwaya ya akina mama wa Usharika wa Mwenge, kwaya ya Vijana ya Usharika wa Mwenge,Kwaya ya Vijana ya Usharika wa Ubungo, kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge, Kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Mwenge, na kwaya ya watoto ya Usharika wa Mwenge
Maharusi wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa
Maharusi wakiwa na wazazi wao.Mpambe wa bwana harusi ni bwana Huruma Mgata na Matron ni Rachel Mgata ambaye ni mke wa Huruma
Picha ya pamoja mbele ya kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge
Baadaye ilifanyika tafrija ya nguvu katika ukumbi wa TBS Ubungo.Pichani juu ni keki iliyoandaliwa kwa ajili ya maharusi
Wageni mbalimbali wakiwa ukumbini TBS Ubungo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akiwa na mumewe Bwana Msangi.Pembeni ni bwana Shujaa
Maharusi wakitambulishwa ukumbini
Maharusi wakikata keki
Maharusi wakilishana keki
Mzazi wa bi harusi akitoa utambulisho
Picha ya pamoja na familia
Katibu wa baraza la wazee wa Usharika wa Mwenge Mzee Kombe, watatu kutoka kwa mzee Kombe ni wazee wa kanisa wa Usharika wa Mwenge Dr Lilian Kitunga na wa mwisho ni mzee mama Laita Ngole
Bwana harusi wakifanya utambulisho siku hiyo
Parish worker wa Usharika wa Mwenge Suzan Mwimbe akitambulishwa
Maharusi wakipakua chakula
Maharusi wakilishana chakula
Bwana harusi ni mwenyeji wa Njombe, kabila ni Mbena na bi harusi ni mwenyeji wa Tabora, kabila ni Mnyamwezi
Mtandao huu unawatakia kila la kheri na baraka tele katika ndoa yao hii!!
(Samahani sana picha hizi zilichelewa kutufikia)
No comments: