MUNGU HUTAKASA NYUMBA ZETU - IBADA KATIKA KANISA LA K.K.K.T - USHARIKA WA MWENGE
Posted by :
Unknown
on :
Sunday, January 19, 2014
0 comments
Ndoa nyingi zina migomo ya kimya kimya na ajuaye ni mke au mme wake.
Akifundisha katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge (misa ya kwanza) mchungaji Enock Kagya (pichani juu) alisema ndoa si tendo la ndoa peke yake ila tendo la ndoa ni kilele cha kumwambia mwenzako kutokana na mema yote ulionitendea; sasa nakupa mwili wangu uutumie utakavyo.Neno lililoongoza mafundisho haya ni Luka19: 1- 10
Mchungaji huyo anayepatikana katika Usharika wa Mbezi Beach alisema kama hakuna ushirika mzuri wa kumtaka mwenzako huko ni kubakana na hakuna mapenzi hapo hata kama unayefanya naye tendo hilo ni mke/mme wako
Kumbuka tendo la ndoa ni takatifu na ni tendo la Mungu mwenyewe
Kwa siku moja mwanaume wa kawaida anazungumza maneno yasiopungua 10,000 na mke wake anataka hayo maneno ayasikie yeye peke yake na si wengine.Ni maneno machache kama yanayojaza karatasi ya A4 tatu hivi.
Lakini mwanamke anazungumza maneno yasiyopungua 25,000 kwa siku moja.Wanaume wengi huwa hawataki kusikiliza maneno mengi.Usipotaka kumsikiliza mwenzako anakua mpweke
Mwanamke akiwa mpweke kunaleta mgogoro katika familia
Mtua ambaye hajawa huru kusema halafu mnataka mfanye naye tendo la ndoa takatifu, unadhani hapo kuna tendo la ndoa kweli kama si kubakana? Aliuliza mchungaji Kagya.
Mwanaume ni kama jiko la makaratasi ambalo linashika moto mara moja wakati mwanamke ni kama jiko la mkaaa ambalo huchukua mda mrefu kushika moto lakini likishika pia huchukua mda mrefu kuzimika.
Tuelewe hivi; kama mama au mwanamke ameweka mambo yake sawasawa na umemsikiliza au mnasikilizana anakua huru; mkifanya tendo la ndoa ambalo ni takatifu mnakua wote mko tayari;kwani tendo la ndoa ni kusikilizana na ni la kisaikolojia.
Mme hupenda kwa kunusa na kugusa tu na akimgusa mwenzake tu huwa tayari wakati mwanamke hupenda kwa kusikia, kubembelezwa, kufurahi,kumchekesha, kuguswaguswa na kupata mambo mazuri mazuri
Siku hizi wengi hupika chakula kwa majiko yaliyozimika (kutokumwandaa mke wake)
Ndoa si kuvumiliana ila ni kufurahishana.Wanandoa inatakiwa waridhishane alimaliza mchungaji huyo
Katika ibada jumapili hii katika Usharika wa Mwenge zilitengwa kwa marika mbalimbali
Ibada ya kwanza ilikua ni ya watu wote (familia nzima) iliyoongozwa na mchungaji Enock Kagya
Ibada ya pili ikawa ya wanandoa Mchungaji Enock Kagya
Ibada ya tatu ikawa ya wagane na wajane iliyoongozwa na bwana Robert toka makao makuu ya Dayosisi
Ibada ya nne ikawa ya vijana iliyoongozwa na mchungaji Ordolus
Saved under :
Habari za Kidini,
Kutoka Madhabahuni
No comments: