Latest News


More

Aishi kwenye handaki kwa miaka minne

Posted by : Unknown on : Tuesday, December 24, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Tunaposikia handaki, fikra zinatupeleka moja kwa moja kwenye vita kwani aghalabu, mahandaki hutumiwa na watu kujificha wakati wa vita.
Hata hivyo, ugumu wa maisha umesababisha baadhi ya watu kuyageuza mahandaki kama makazi ya kuishi.
Ni katika Barabara ya Sam Nujoma, natoka Ubungo kuelekea Mwenge, nashuka mita chache kabla ya kufika Mlimani City, naingia katika pori lililo nyuma ya Ukumbi wa Mlimani City.

Hakuna njia maalumu ya kuingia katika pori hili. Hatua kwa hatua napita katikati ya vichaka na nyasi ndefu, hatimaye nafika katika eneo tofauti. Ni kama bustani iliyotengenezwa na mbunifu wa hali ya juu.
Miti imefyekwa kwa utalaamu wa hali ya juu, baadhi ya vichaka vimepunguzwa kwa umahiri na kutengeneza umbile zuri mfano wa maua yaliyotengenezwa. Lakini, mwisho kabisa wa mandhari hii kuna mianzi imelazwa chini na pembeni kuna shimo.
Shimo hilo ndilo handaki analoishi Chacha Makenge, kijana mwenye umri wa miaka 36, mzaliwa wa Mugumu Wilaya Serengeti Mkoa wa Mara kwa muda wa miaka minne sasa.
Hata hivyo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Makenya Maboko anasema kuwa hana taarifa zozote kuhusu Makenge kuishi katika eneo hilo.
“Sina taarifa, wewe ni mtu wa kwanza unanipa habari hizi, ngoja nilifanyie kazi,” anasema Profesa Maboko

Jirani na handaki hilo namkuta Makenge akifyeka majani kwenye bustani yake. Ananikaribisha na tunaingia katika handaki hilo. Ni shimo refu, kwani tunatakiwa kushuka ngazi tatu kubwa kwenda chini. Ndani kuna kitanda cha kamba na miti kilichofunikwa kwa magunia na shuka kadhaa.
Ukuta ambao ni udongo, umechongwa mithili ya meza ndogo ambayo Makenge ameweka kioo, kitana, boksi lenye dawa mbalimbali na mswaki.
Upande wa kulia wa handaki hili kuna misumari iliyopigiliwa katika ukuta huo ambapo Makenge ametundika makoti na suruali, ambazo bila shaka ni zake.
Upande wa kushoto, Makenge kwa kutumia ukuta huo huo, ametengeneza meza nyingine ambayo imewekwa chupa za plasitiki za maji ya kunywa. (Source: Mwananchi Communication)

No comments:

Leave a Reply