Latest News


More

KIPAIMARA MWAKA WA PILI WAAGWA NA WENZAO KANISA LA K.K.K.T - USHARIKA WA MWENGE

Posted by : Unknown on : Thursday, December 5, 2013 0 comments
Unknown

Jana katika kanisa la K.K.K.T - Usharika wa Mwenge wanafunzi wa kipaimara mwaka wa pili  waliagwa rasmi na wenzao wa mwaka wa kwanza


Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika katika chumba cha darasa la Sunday school na kipaimara ilihudhuriwa pia na mama mwenyekiti wa malezi wa Usharika wa Mwenge mama Lema, mwinjilisti wa Usharika huo mama Mwigune na Parish worker wa Usharika huo Suzane Mwimbe ambaye ndiye aliyekua mwandaaji wa hafla hiyo.Pia wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa pili walihudhuria.Pamoja na vinywaji pia waliandaa keki kama alama ya kuagana na wenzao kama inavyoonekana pichani juu
 Pichani juu na chini wanafunzi hao wakiwa kwenye hafla hiyo


 Parish worker Suzan Mwimbe (ambaye alikua kiongozi wa hafla hiyo) akiongoza hafla hiyo hapo jana jioni
 Mama Mlezi wa malezi wa Usharika wa Mwenge ambaye pia ni mwenyekiti wa malezi wa jimbo la kaskazini akisoma neno la Mungu la kuwaasa wanafunzi wa kipaimara wa mwaka wa pili

 Hatimaye wakati wa keki ulifika ambapo mwanafunzi mmoja wa mwaka wa kwanza na mmoja wa mwaka wa pili walikata keki kwa pamoja

 Kisha mwanafunzi wa mwaka wa pili alimlisha keki mama wa malezi
 Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza akimlisha mwinjilisti wa Usharika keki

 Kisha nao walipata nafasi ya kulishana keki kama alama ya kutakiana maisha mema
 Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakilishana keki na wale wa mwaka wa pili
 Keki zinaendelea kama kawaida
 Kisha wakapata nafasi ya kufanya cheers na meza kuu
 Hatimaye Caroline Munuo alipata nafasi ya kusema neno kwa niaba ya wanafunzii wa mwaka wa pili waliokua wanaagwa
 Pia Jenifa Emanuel wa mwaka wa kwanza naye alitoa neno  kwa niaba ya wenzake
Mwisho Evarada Simon wa mwaka wa pili alifunga hafla hiyo kwa sala

Wanafunzi wa mwaka wa pili wanatarajiwa kupata kipaimara siku ya jumamosi wiki hii
Mtandao huu unawatakia kila la kheri katika siku yao hiyo muhimu

No comments:

Leave a Reply