KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUMILIKI
Posted by :
Unknown
on :
Monday, December 2, 2013
0 comments
KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU KATIKA KUMILIKI
Mwanadamu aliyeumbwa na Mungu kila siku lazima awe na kiongozi.Mtu hawezi kuongozwa na viongozi wawili kwa wakati mmoja.Ni lazima awe na kiongozi mmoja tu .
Akifundisha katika ibada ya jumapili hii katika Usharika wa Mwenge wa kanisa la K.K.K.T mwinjilisti Prosper Mgaya alisema kuongozwa na nani kati ya viongozi wawili ni chaguo langu/lako au la mtu husika.
Ni uamuzi wako kuamua uongozwe na nani kati ya kuongozwa na mwili au na roho Mtakatifu
Katika mafundisho hayo bwana Mgaya alisoma neon toka Warumi 8: 12 – 14
Katika mstari wa 14 – “ Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’
Katika uongozi kuna anayeongoza na anayeongozwa.Kiongozi yoyote hawezi kuongoza kama Yule anayemuongoza hajakubali kuongozwa
Yohana 10:27 “Kondoo wangu waisikia sauti yangu;name nawajua , nao wananifuata”
Mungu ametupa Roho Mtakatifu atuongoze.Si rahisi kuongozwa na Roho takatifu.Lakini ukiamua ni rahisi.Ukiamua chukua hatua
Kuongozwa na Roho Mtakatifu ni process, si jambo la siku moja.
Ni uamuzi wa mtu mwenyewe wa ndani ya moyo wake.Ila kumbuka kuwa kusimama, au kudondoka na kuinuka ni maisha ya mtu Yule amliyeamua kumfuata Roho mtakatifu
Bwana Mgaya alitoa mfano wa ,motto mdogo anayejifunza kusimama.Mara nyingi hua anadondoka , na kuinuka, anadondoka na anainuka na kusonga mbele na mwishowe husimama kabisa na kutembea
Ikiwa kudondoka kwake kutamkatisha tama na kuacha kujaribu, basi hataweza kutembea kamwe
Hali kadhalika mkristo anapoanguka na kusimama na kusonga mbele ndio huimarika kiroho na mwishowe kushinda na hatimaye ni urithi wa uzima wa milele, alisisitiza bwana Mgaya
Ufuasi wa kumfuata Roho Mtakatifu ni safari ambayo inahitaji msaada.Na msaada unapatikana kwa Yesu Kristo pekee
Ukiamua , tii na Yesu Kristo atakuwezesha
Ukishaamua kuwa mfuasi wa Yesu Kristo utakuwa tayari kufanya yale Roho Mtakatifu anayotaka uyafanye alimaliza bwana Mgaya
Katika ibada hiyo iliongozwa na Parish worker wa Usharika wa Mwenge Suzan Mwimbe na mchungaji wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi
No comments: