Unaweza kuutuma kwenye ukurasa wetu wa Bofya Facebook Bofya bbcswahili na kisha nitauweka hapa kwenye mtandao wetu waBofya bbcswahili.com. Je uko Afrika Kusini? nini kinajiri huko mbali na misa hii kufanyika?
13:23
13:14 William Francis kupitia ukurasa wa Bofya facebook akiwa mjini kigali Rwanda, anasema kuwa Dira ya vijana ya kizazi hiki tukubali imepotezwa na viongozi wa sasa, hakuna kijana atakayerithi urithi wa Mandela, hapa tuseme tu, kisha tuendelee na yetu ya siku zote. Ukitazama dunia ya leo upande wa kufundishana maadili ni dini zilizoongezeka angalia ndiyo moto wa vijana unapaa juu kupita sayari zote, useme tuje tubadilike kwa lipi Obama?
Rais Barack Obama, Jacob Zuma na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
12:53 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aanza kuwahutubia wananchi waliofika kwa misa ya wafu ya Mandela
12:48 Stanley Kisaka akiwa nchini Tanzania kupitia ukurasa wa Bofya Facebook anasema kuwa ni kweli kabisa hatutakuwa na viongozi wazalendo kama MANDELA zaidi ya kupata viongoz wanaojipenda wenyewe MUNGU IBARIKI AFRIKA!!!!!
12:00 Obama: ''Hatutawahi kuwa na kiongozi kama Mandela duniani tena. Lakini nataka kuwashauri vijana kote Afrika na duniani kote kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo zake Mandela.''
11:51 Obama :'Kumbukumbu za Mandela hunifanya kila siku kutaka kuwa mtu mwema na nataka kuwashauri vijana kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo za Mandela'
1135 Obama: ''Asanteni sana kwa kuturuhusu kumuenzi Nelson Mandela, alikuwa mkombozi aliyetetea demokrasia na anaweza tu kufananishwa na marehemu Mahatma Ghandi. Ni vyema kumkumbuka Mandela kama mtu aliyejitolea sana na hakuogopa kushauriana nasi kuhusu maoni yake na hisia zake na kwa sababu Mandela aliweza kukubali kuwa mtu wa kawaida mtu ambaye aliweza kufanya makosa kama mwanadamu mwengine yeyote ule.''
Barack Obama kwenye misa ya wafu ya Mandela
11:31...Rais wa Marekani Barack Obama aanza kuhutubia wanachi wa Afrika Kusini wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
11:15.....Dlamini Zuma, 'Tunamuenzi Madiba, alikuwa shujaa aliyekuwa tayari kusikiliza maoni ya watu wengine licha ya kukinzana na yake. Ni shujaa wa Afrika ambaye alijitolea kuikiomboa Afrika na juhudi hizo hazikuwahi kumuondoka daima hadi kifo chake.''
11:12 am Mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma anahudhuria umati wa watri kwenye misa hiyo
11:09 am: Taylor Peter Kutoka Dodoma Tanzania ameandika kwenye ukurasa wa Bofya facebook wa Bofya bbcswahili- amesesma Mungu aiweke pahala pema roho ya shujaa na mkombozi wa Afrika. R.I.P MADIBA
11:05 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemaliza kuhutubia umati wa watu waliokusanyika kwenye misa ya wafu ya Mandela
Ban Ki moon akihutubia watu uwanjan
11:03 am Ban Ki Moon: ''Ni Muhimu sote kuendeleza sera za shujaa wetu Mandela''
11:00 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anahutubia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa FNB
No comments: