Maelfu wamuaga shujaa wa Afrika Mandela
Posted by :
Unknown
on :
Tuesday, December 10, 2013
0 comments
Zaidi ya marais tisini wameungana na wananchi wa Afrika Kusini katika misa ya wafu ya Nelson Mandela na kusimulia kumbukumbu zao kwa Shujaa huyo wa Afrika.
Akiongea kwenye mkusanyiko huo mjini Soweto, Rais wa Marekani Barack Obama alimtaja Mandela kuwa shujaa na mkombozi wa Afrika na shujaa shupavu kuwahi kuonekana katika karne ya ishirini.
Alisema maisha ya Mandela lazima yawe mfano mzuri kwa dunia nzima hasa vita alivyopigania kuhakikisha utu wa watu unaheshimiwa.
Jamaa za Mandela wamemtaja baba yao Mandela kama mtu aliyetaka watu kuwa sawa.
Mmoja wa wajukuu wa Mandela alikariri shahiri la kusisitiza mshikimano wa watu. Obama alishangiliwa ingawa Rais Jacob Zuma anayehutubia wananchi alizomewa mara kwa mara.
Uwanja ambako misa hiyo inafanyika, haukujaa watu kutokana na mvbua kubwa iliyonyesha.
TAARIFA YA AWALI
Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini.
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia watakaohutubia muhadhara huo.
Familia ya Hayati Mandela
Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela .
Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.
Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela:
Viongozi wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
* Rais wa Marekani Barack Obama
* Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
* Rais wa Cuba Raul Castro
* Rais wa Ufaransa Francois Hollande
* Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
* Rais wa Brazil Dilma Rousseff
* Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Watu wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita.
Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
Saved under :
Neno la leo
No comments: