Je wazijua sheria nne za kiroho?
Sheria hizi Nne za kiroho ni njia za kushiriki habari njema za wokovu
upatikanao kupitia imani ndani ya Yesu Kristo. Ni njia moja rahisi ya
kupanga habari muhimu katika injili kwa sehemu Nne.
Ya kwanza kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Mungu anakupenda na ana
mpango wa ajabu juu ya maisha yako.” Yohana 3:16 yatwambia, “Kwa maana
jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili
kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 10:10
yatupa sababu ya kuja kwake Yesu, “Mimi nalikuja ili wawe na uzima,
kisha wawe nao tele.” Ni kitu gani kinachotuzuia na upendo wa Mungu? Ni
kitu gani kinacho tupinga kupata uzima ulio tele?
Ya pili kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Hali ya Utu wa mwanadamu
inachafuliwa na dhambi na hivyo basi kutengwa na Mungu. Kwa matokeo haya
basi, hatuwezi kamwe kuufahamu mpango wa ajabu alio nao Mungu juu ya
maisha yetu.” Warumi 3:23 inatuhakikishia habari hii, “Kwa sababu wote
wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Warumi 6:23
inatupatia madhara ya dhambi, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti.”
Mungu alituumba ili tukaweze kuwa na ushirika naye. Hata hivyo hali ya
Utu/Ubinadamu ilileta dhambi katika dunia, na hivyo basi kutengwa na
Mungu. Tumeharibu uhusiano pamoja naye ambao Mungu alikusudia tukaupate.
Je, suluhisho ni nini?
Ya tatu kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Yesu Kristo ndiye toleo
la Mungu pekee kwa ondoleo la dhambi zetu. Kupitia kwa Yesu Kristo,
tunaweza kusamehewa dhambi zetu na kurudisha ushirika wa haki na Mungu.”
Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu
sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye
dhambi.” Wakorintho 15:3-4 inatufahamisha kinachotupasa kujua na kuamini
ili tupate kuokoka, “……ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,
kama yanenavyo maandiko, yakuwa alizikwa; ya kuwa alifufuka siku ya
tatu, kama yanenavyo maandiko….” Yesu mwenyewe akiri yakwamba yeye ndiye
njia ya pekee ya wokovu katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli,
na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.” Je, ninawezaje
kupata kipawa hiki kikuu cha wokovu?
Ya Nne kati ya sheria hizi Nne za Kiroho ni, “Ni sharti tuweke imani
yetu ndani ya Yesu Kristo kama mwokozi ili tukaweze kupokea kipawa cha
wokovu na kujua mpango wa ajabu wa Mungu juu ya maisha yetu. Yohana 1:12
inatuelezea hivi, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika
watoto wa Mungu. “Matendo16:31 inazungumzia kwa ufasaha zaidi, “Mwamini
Bwana Yesu nawe utaokoka!” Tunaweza kuokolewa kwa neema peke yake, kwa
njia ya imani pekee, ndani ya Yesu Kristo pekee (Waefeso 2:8-9).
Ukiwa unataka kumwamini Yesu Kristo kama mwokozi wako, sema maneno
yafuatayo kwa Mungu. Kusema maneno haya haitakuokoa, lakini itawezekana
kwa kumwamini Kristo!Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako
kwake na kum shukuru kwa kukupea wokovu. “Mungu, ninajua yakwamba
nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo
akaichukua adhabu niliyo stahili ili kwa kumwamini yeye, nipate
kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani
yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako kuu na kwa msamaha-
karama ya uzima wa milele! Amina!”
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo,
tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: