UMUHIMU WA KUWEKA NADHIRI NI KUIONDOA KWA WAKATI
Neo Kuu 1 Samwel 1 :10-11
Neno la waraka Kol 1:16-17
Zaburi 123
Umuhimu wa kuweka nadhiri kwaMungu ni kiiondoa kwa
wakati.Akihubiri katika ibada ya
jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge mchungaji Mchomvu amesemanadhiri ni ahadi ambayo mtu anaweza kutoa
Akitoa mfano katika kitabu cha 1 Samwel1_10-11 amesema Anna
alikua mke wamkubwa wa Elikana na mke mdogo aliitwa Penina
Hannah hakujaliwa kupata motto ila Penina alikua na watoto.Elikana
aliwapenda wake zake wote ila alimpenda Penina zaidi kwa kua alikua na watoto
Hawa wake wawili hawakua wakipatana kwa kua Penina
alimchukia zaidi Hannah kwa kukosa watoto.Mara nyingi alikua anamchokoza na
kumuudhi Penina hata wakati wakienda ibadani.Lakini Hannah aliendelea kuwa
magotini kwa Mungu na kuomba kwa bidii na akaweka nadhiri kwa bwana akiomba kwa
machozi na kulia na akasema kama bwana atamjalia kupata motto basi nadhiri yake
kwa bwana ni kumtoa huyo motto amtumikie Bwana
Hannah alitoa ahadi yake hii toka rohoni
Biblia inasema ili nadhiri iwe na maana ni lazima ukumbuke
kuitoa kwa wakati au kuitimiza kwa wakati
Mungu hupendezwa sana na watu wanaoweka nadhiri na huwa
hakawii kuitimiza kwa Yule aliyeiweka alisema mchungaji Mchomvu
Mungu aliitimiza nadhiri ya Hannah na Hannah naye alitimiza
nadhiri yake kwa bwana kwa kumtoa motto wake Samwel amtumikie bwana
Inawezekana unaweka nadhiri lakini je; ina tija kwa bwana?
Je unaweka nadhiri kwa mahitaji yako binafsi au kwa manufaa ya Mungu na
wanadamu
Mungu anapenda yeye awekae nadhiri ambayo ina tija kwa bwana
na wanadamu pia
Ondoa nadhiri yako mapema mara tu baada ya kuipata
Tafakari nadhiri yako uliyoiweka kwa bwana, je
ulikwishaitoa? Kama bado hujachelewa itoe sasa
Upendo wa Mungu utadhihirika kwako pale tu utakapotoa na
kuitimiza nadhiri kwa bwana alihitimisha mchungaji MchomvuIbada hiyo iliongozwa
na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi
Watoto wa shule ya jumapili wa Usharika wa Mwenge wakiwa
katika ibada ya jumapili
Mwaliku wa shule ya jumapili Eliajua Geofrey (pichani juu) akiongoza ibada hiyo ya leo
Wakristo wa Usharika wa Mwenge jumapili ya leo wameshiriki
chakula cha bwana katika ibada zote tatu zinazofanyika katika ibada za kila
jumapili
Pichani juu na chini washarika wakishiriki chakula cha bwana
No comments: