Latest News


More

YESU KRISTO ANAINGIA YERUSALEM KWA SHANGWE

Posted by : Unknown on : Sunday, April 13, 2014 0 comments
Unknown

 Sikuku uya mitende ni sikukuu kubwa sana kwa wakristo ambayo tunakumbuka mchakato mkubwa wa ukombozi wetu
Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T U sharika wa Mwenge mchungaji kiongozi wa Usharika huo Kaanasia Msangi (pichani juu) alisema sikukuu ya mitende ni siku ambayo Yesu Kristo aliingia Yerusalem kama mfalme na safari ya mwisho ya kifalme
Safari hii Yesu Kristo anaingia Yerusalem akijua si kama alivyowahi kuingia hapo nyuma
Mathayo 20: 17 – 19
Yesu aliju anaenda kuhitimisha utumishi wake wa ukombozi wa mwanadamu
Yerusalem ilikua na pilika pilika ya maandalizi wa Pasaka ya Wayahudi
Yohana 12:12
Mji ulikua na wageni wengi toka sehemu mbalimbali kama vile Kapernaumu, Yeriko, Nazareth, Tiro na Sidon ink
Watu wengi hao walimfaham Yesu na miujiza mingi ambayo aliifanya kama vile uponyaji, kuondolewa mapepo n k na watu hao wote walikua Yerusalem
Yohana 12 inasema wengi wao ni wale walioacha dini zao za asili na kumfuata Yesu haswa baada ya ule muujiza wa kumfufua Lazaro
Yesu Kristo anawatuma wanafunzi wake wakamlete punda aiyefungwa na ambaye hajatumika bado, na aliwaambia wakiuliza wanampeleka wapi wasema bwana ana haja naye na watamrudisha
Yesu alitaka wajue kwamba yeye ni Mungu katika Israel nay eye ni yote katika yote

Yesu anatumia punda ili atomize unabii uliotolewa kabla na manabii Zakaria 9:9
Jambo hili likikua na mambo mengi ya kujifunza
Tukio la Yesu kuingia kama mfalme wengi walighadhabika haswa wakuu wa makuhani na waandishi
Mwana punda alipoletwa wanafunzi walimtandikia nguo zao na mavazi yao na Yesu alipita juu yake na wale ambao hawakua na nguo walikata majani ya mitende na kuyatandaza njiani ili Yesu aweze kupita huku wakiimba Hossana Hossana mbarikiwa
Hiiilikua ni kutimiza unabii ulionenwa na manabii na safari hii ya Yerusalem ilienda hadi ikulu ya Mungu
Katika somo hili tunajifunza mambo makuu yafuatayo;
1.       Safari ya bwana Yesu ambayo ilikua safari ya kimasihi ya kukamilisha utumishi wake hapa duniani.Yesu alifundisha, alihubiri na aliandaa mitume na kuokoa watu
2.       Tunajifunza kwamba Yesu anajua mambo yote kwa maana yeye ni Mungu kweli, hawezi kufichwa jambo lolote lile .Hakuna jambo unaloweza kumficha Mungu, mnaweza kuwaficha wanadamu lakini si kumficha Mungu Ufunuo 2: 2-3
3.       Vyote tulivyo navyo na sisi wenyewe ni mali ya bwana , mali , dhahabu, na sisi wenyewe ni mali ya Bwana ,akitaka anachukua wakati wowote autakao
4.       Wakuu wa makuhani na waandishi walikua na hasira juu ya Bwana Yesu. Hata leo hii kuna watu wanaojitahidi sana kuzima vipawa vya watu wengine na kuwakatisha tama.Sisi kama wakristo hatutakiwi kuzima taa au karama za wengine ila tuwatie moyo ili tusonge mbele katika kazi ya Bwana
Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji Fue




No comments:

Leave a Reply