Kuna hofu kuwa raia wakristo kutoka Syria wametekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State.
Duru kutoka kwa jamii hiyo sasa inathibitisha kwamba zaidi ya raia 200 walitekwa nyara Jumanne baada ya vijiji kadhaa kushambuliwa kazkazini mwa Syria.Wengi wa waliotekwa nyara ni wanawake na wazee.
Wakati huo huo, mapigano yangali yakiendelea katika maeneo yaliyoko karibu na mji wa Hassaka.
Kuna taarifa zinazosema kuwa makanisa yameteketezwa moto na kundi la IS katika vita hivyo vikali kati ya wanamgambo hao na makabila ya Wakurdi wanaoungwa mkono na wakristo wenye silaha.
Taswira kamili ya mkasa uliowakumba wakristu hawa wa Syria ndio mwanzo unaanza kujitokeza.
Lakini kikundi cha wapiganaji wa kikristu kimetoa madai kuwa idadi hiyo ni kubwa hata zaidi ya hiyo.
Kimedokeza kuwa zaidi ya watu mia tatu hamsini wametekwa.
Huku hayo yakiarifiwa waumii wengine wa kikristu wameanza kukimbia avijiji vyao wakihofia kushambuliwa na wanamgambo wa Islamic State.
Na bado vita vinaendelea huku waislamu hao wakikabiliana na waasi wa kikurdi pamoja na washirika wao wa kiksristu katika mji wa Hassaka.
No comments: