Enugu, Nigeria.
Mchungaji Timothy Ngwu (53) pichani juu aliyezungushiwa duara wa nchini Nigeria amewapa mimba zaidi ya waumini wake 20 kwa madai ya kwamba Roho Mtakatifu alimwabia afanye mapenzi nao.
Kiongozi huyo wa kanisa la Vineyard Trinity ambaye hivi sasa anashikiliwa na
polisi nchini humo, alifanya kitendo hicho kwa waumini wanawake ambao wameolewa
na wasichana wadogo ambao hawajaolewa.
Akizungumza na gazeti la NAIJ na baadaye kunukuliwa na gazeti la Jewsnews la
nchini humo, Msemaji wa Kituo cha Polisi cha Enugu ambapo Ngwu anashikilikiwa,
Ebere Amaraizu alisema wamemkamata kiongozi huyo kwa kosa la unyanyasaji wa
kijinsia kwa waumini wanawake.
“Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba alilazimika kufanya hivyo kwani hayo
yalikuwa maono ya kinabii na alifanya hivyo kwa sababu alikuwa anatii maono
aliyoonyeshwa na Mungu. Maono ambayo ni kumpa mimba mwanamke yeyote ambaye Mungu
amemchagua na kumwonyesha yeye kwa njia ya Roho Mtakatifu bila ya kujali kama
huyo ameolewa au la,”alisema Amaraizu.
Aliongeza: “Mwanamke akijifungua atakuwa akiishi kanisani pamoja na mtoto kwa
maisha yao yote.”
Mchungaji Ngwu akifanya huduma kwenye kanisa lake
Mke wa mchungaji huyo ambaye baadaye alimfukuza, Veronica Ngwu ndiye
aliyeenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi baada ya kuchoshwa na tabia hiyo
hasa alipofikia hatua ya kumpa mimba mtoto wa kaka yake.
Ndugu wa karibu wa mchungaji huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema
walimuonya kaka yao juu ya tabia hiyo, lakini hakutaka kuwasikiliza huku akidai
kuwa anatekeleza agizo la Mungu.
“Hiki kilichompata kaka yetu ni hasira kutoka kwa Mungu kwa sababu tulimuonya
lakini hakutaka kutusikiliza. Amekuwa mtemi hapa kwetu, anawapa wanawake mimba
hovyo hovyo kwa kutumia jina la Mungu halafu ukimuonya anasema tunamuonea
wivu,”alisema.
Alilalamika kuwa, Ngwu amejimilikisha sehemu ya shamba la familia yao na
kufanya kanisa lake ambalo anatumia kwa kufanyia maovu hayo kwa jina la
Mungu.
“Alimfukuza mke wake ambaye amezaa naye watoto watatu halafu sasa hivi
anafanya kazi ya kuzaa na kila mwanamke bila kujali kama ameolewa au hajaolewa
wengine ni wasichana wadogo…angalia uwanja mzima umejaa watoto wa umri na jinsia
tofauti, “alilaumu.
Ndugu huyo alisema, inashangaza kuona mtu na elimu yake anafanya vitendo kama
hivyo
(Source: Mwananchi Communication)
(Source: Mwananchi Communication)
No comments: