Latest News


More

MAMA MKRISTO ANATAKIWA AWEJE?

Posted by : Unknown on : Friday, October 11, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :

Bibilia inasema nini kuhusu kuwa mama Mkristo?
Jibu: Kuwa mama ni jukumu la muhimu sana ambalo Mungu alilichagua kulipa wamama wengi. Mama Mkristo ameambiwa kuwa awapende watoto wake (Tito 2: 4-5), katika sehemu ili asilete shutuma kwa Mungu na Mwokozi ambaye kwa jina lake abeba jukumu.

Watoto ni tuzo kutoka kwa Bwana (Zaburi 127:3-5). Katika Tito 2:4, neno la Kiyunani philoteknos laonekana kuwaambia wamama kuwapenda wana wao. Hili neno linadhihirisha “upendo wa mama” maalumu. Dhana ambayo yotoka katika maneno haya ni ile ya ulezi wa watoto wetu, kwa upendo kuwakumbatia, kutimiza mahitaji yao, kwa ukarimu kufanya urafiki na kila mmoja kama tuzo la ajabu kutoka kwa Mungu.


Mambo mengi yameamriwa kwa wamama Wakristo katika neno la Mungu:

Kuwa karibu- Asubuhi, mchana na hata usiku (Kumbukumbu La Torari 6:6-7)
Husisha- kutangamana nao, kujadiliana nao, kuwaza nao na kusukuma maisha pamoja (Waefeso 6:4).
Kuwafundusha- maandiko na mitazamo ya Kibibilia (Zaburi 78:5-6; Kumbukumbu La Torati 4:10; Waefeso 6:4)
Kuwaelekeza- msaidie mtoto kukuza ujuzi na kugundua uwezo wake (Methali 22:6) na karama za roho (Warumi 12:3-8 na 1 Wakorintho 12).
Kurudi- kuwafunndisha kumcha Mungu, kuwa na msimamo kila wakati, kuwa wa upendo na wenye msimamo imara (Waefeso 6:4; Waebrania 12:5-11; Methali 13:24; 19:18; 22:15; 23:13-14; 29:15-17)

Kutunza- kuwapa mazingira ya usemi wa kila wakati, uhuru wa kuanguka wanachokifanya, kuwakubali, upendo usio wa masharti (Tito 2:4; 2 Timotheo 1:7; Waefeso 4:29-32; 5:1-2; Wagalatia 5:22; 1 Petero 3:8-9).
Kuwa mfano mwema kwa maadili- kuishi na pia  kuwa kielelezo kutoka kwa mtoto ataweza kujifunza kwa “kushika” hizi tabia za kuishi maisha ya uungu (Kumbukumbu La Torati 4:9, 15, 23; Methali 10:9; 11:3; Zaburi 37:18, 37).
Bibilia kamwe haitaji kuwa kila mwanamke lazima awe mama. Ingawa, huwa yasema kwamba wale ambao Mungu amewabariki kuwa wamama lazima wachukue majukumu yao bila mchezo. Wamama wana  jukumu la ajabu na la muhimu katika maisha ya watoto wao. Uzazi wa mama sio wa kuchosha au kazi isiyofurahisha. Vile mama anavyomzaa mtoto wakati wa uja uzito, na kama vile mama anavyomnyonyesha na kumlea mtoto akiwa mchanga, kwa hivyo wamama wanatekeleza jukumu linaloendelea katika maisha ya watoto wao, hata kama wamefika umri wa kubalehe, ujana, au utu uzima wakiwa na watoto wao. Huku ikiwa ni jukumu la mama lazima libadilishwe na liannziishe, upendo, ulezi, utunzi, na utiaji moyo mama anaowapa watoto kamwe usikome.

No comments:

Leave a Reply