Mashindano ya Uimbaji katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) - DMP ngazi ya Jimbo la Kaskazini yanafanyika kesho katika kanisa la Usharika wa Mbezi Beach
Katika mashindano hayo yatakutanisha kwaya ambazo zilishinda kwa nafasi ya kwanza mpaka ya tano katika ngazi ya kanda ambayo yalifanyika katika sharika mbili ambazo ni Usharika wa Kunduchi na Mwenge jumamosi iliyopita
Katika kituo cha Kunduchi mshindi wa nafasi ya kwanza alikua kwaya ya Usharika wa Kijitonyama wakati katika kituo cha Mwenge mshindi alikua kwaya ya Usharika wA Bunju
Washindi wengine katika kituo cha Kunduchi watakaowakilisha kwenye ngazi ya jimbo ni;
Mshindi wa pili ni kwaya ya Usharika wa Manzese
Mshindi wa tatu ni kwaya ya Usharika wa Kinondoni
Kwaya ya Usharika wa Kinondoni wakiimba jumamosi iliyopita
Na mshindi wa tano ni kwaya ya Usharika wa Kunduchi
Washindi wengine katika kituo cha Mwenge watakaowakilisha mashindano ya ngazi ya jimbo ni;
Mshindi wa pili ni kwaya ya Usharika wa Wazo Hill
Mshindi wa tatu ni kwaya ya Usharika wa Mwenge zilizofungana na kwaya ya Usharika wa Mbezi Beach
Mshindi wan ne ni kwaya ya Usharika wa Magomeni ambayo ilifungana na kwaya ya Usharika wa Sinza
Na mshindi wa tano ni kwaya ya Usharika wa Msasani
No comments: