Latest News


More

ADUI WA MKRISTO NI NANI?

Posted by : Unknown on : Friday, May 31, 2013 0 comments
Unknown
Saved under : ,

ADUI YAKO  NI NANI?
Ingawa tunasema Mkristo anatakiwa aishi kwa amani na watu wote (soma Warumi: 12:18), maana ya kuunganika kwake na Yesu Kristo ni kwamba watu wengine watamchukia.
Kwa hiyo Mkristo huyu atakuwa na maadui wengi.Na ujue kwamba adui yoyote  yule wa Mkristo ni adui wa Mungu, na maadui wa Mungu ni maadui wa Mkristo vile vile.(Kut.23: 22;Zab 37: 20;55:2-3;Mt 10:22,36)

Hata hivyo tunaaswa na Yesu Kristo kwamba Mkristo anapaswa kuwapenda adui zake na kuwatendea mema watu wanaomchukia (Mt 5:44;Lk 6:27)
Biblia inaeleza habari za maadui wengine kuliko wanadamu wenzetu, mfano ni 
Shetani,maadui na mamlaka mbaya ya kiroho.
Lakini Kristo alishinda uadui wote kwa njia ya kufa na kufufuka kwake,na siku ya ushindi wake wa mwisho atawaangamiza maadui wote mpaka milele (Mt 13:39;Lk 10:18;       Kol 2:15)
 (Kichila Tumaini S -  2013)

No comments:

Leave a Reply