Mwinjilisti Godilizen Moshi (pichani juu) akihubiri kwenye ibada ya kanisa la K.K.K.T Usharika wa
Mwenge alisema Uchumi ni njia mojawapo mkristo anatakiwa kutumia katika
kumtumikia Mungu
Mtumishi huyo alisema katika majuma matatu mfululizo kuanzia
jumapili hii atafundisha jinsi mkristo anatakiwa kutumia fursa ya uchumi katika
kumtumikia Mungu
Alisema
1.Mhubiri 3: 1 – Kila fursa ya maisha ya mwanadamu imefungwa
ndani ya majira na wakati
Kuna umri ukifika huwezi kufanya mambo Fulani hata kama
unataka.Alitoa mfano wa elimu huwezi kuanza elimu ya msingi ukiwa na miaka 55
kama kwa kufanya hivyo ni ili ukimaliza shule uweze kuajiriwa kufanya kazi,
kwani utamaliza shule umri wa kuajiriwa ukuwa umekwisha
Lazima ujua hata uchumi wako umefungw akwa majira na wakati
husika
Aliyebarikiwa katika uchumi ametumia fursa yake vizuri
2.Kusudi la Mungu ni mumfanikisha mwanadamu katika maeneo
yake yote
Isaya 48: 17
Mungu amekusudia mwanadamu kufanikiwa kwani neon la Mungu
linasema hivyo katika Isaya
Faida uliyopata , unatembea katika misingi ya Mungu
alivyokupa?
Ungu anavyokufanikisha unatakiwa na wewe umshirikishe katika
mafanikio yako alisisitiza mwinjilisti Moshi
3.Uchumi ni maarifa na ufahamu wa kutumia rasilimali katika
kuzalisha
- 1 Falme 17: 10-16
Habari ya mwanamke wa Sarepta na Eliya
Mwanamke ana kiasi kidogo tu cha chakula lakini Eliya nabii
anaona fursa aliyo nayo mwanamke huyo
Nabii haoni chakula kidogo bali anaona zaidi ya mwanamke
huyu anavyoona
Mwisho tunaona mwanamke huyu anatumia fursa yake sawasawa na
anakula na hata kusaza mpaka hali ya njaa inavyoisha kwenye mji aliokua anaishi
JE UNAITUMIAJE FURSA ULIYO NAYO WEWE KAMA MKRISTO? ALIULIZA
MWINJILISTI SHAYO
Picha ya juu na chini waumini wakiwa kwenye ibada ya kwanza kwenye usharika wa Mwenge
Team ya kusifu na kuabudu ikihudumu kwenye ibada ya kwanza
No comments: