Ibada ya jumapili ya leo katika Usharika wa Mwenge imefanyika
leo katika kanisa la Kiinjili la Kilitheri Tanzania (K.K.K.T).
Katika ibada ya leo iliyoongozwa na Mwinjilisti wa Usharika
huo mwinjilisti Mwigune na mahubiri yaliongozwa na mchungaji Kiongozi wa
Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi
Akihubiri katika ibada hiyo mchungaji Kaanasia alisoma neno lenye
kichwa kinachosema “MWENYE KUVUMILIA MPAKA MWISHO NDIYE ATAKAYEOKOKA”….Luka 12:35
– 40
Mchungaji Kaanasia alisema kuvumilia ni kumngoja bwana wetu
Yesu Kristo
Kabla Yesu Kristo alisema namna ya kuutafuta ufalme wa Mungu
kwanza na hayo mengine yote mtazidishiwa
Mungu amewapa ufalme hivyo msiogope kwani Mungu ni muweza wa
yote
Aya ya 35 – 36 – Maandalizi ya ufalme ujao .Watu wasiishi
kama wenyeji kwani wenyeji wetu sio katika ulimwengu huu; tuishi kama wapitaji
tuu
Tufanye bidii katika kufanya kazi; maisha yetu yawe ya
utambuzi wa majira na nyakati.
Taa zetu ziwe zinawaka na tuwe na macho yanayoona
alisisitiza mchungaji Kaanasia
Utayari huu uwe katika kufanya kazi ya kuutafuta ufalme wa
Mungu na vyote vingine Mungu atatuzidishia
Aya ya 37 – 38 – Uheri wa wale walio tayari.
Saa ya kurudi kwa ufalme wa Mungu hakuna ajuaye;hata malaika
wa mbinguni hawajui
Mungu anatuhimiza kutokuchola kwa habari ya kumsubiri mwana
wa Mungu
Tuishi maisha ya kujikana , maisha ya kujitoa na ni hatari
kujitoa katika uvumilivu
Yesu Kristo alisema mtasikia vita huko na huko;ndugu na
ndugu watagombana.Muonapo hayo basi mjue ule mwisho umekaribia
Huu ni wakati wa kujiandaa kumlaki Bwana harusi ambaye ni
Yesu Kristo kwani muda wa kurudi kwake umekaribia
Atakayevumilia mpaka mwisho huyo ndiye atakayeokoka
alimalizia mahubiri yake mchungaji Kaanasia Msangi
Katika Usharika wa Mwenge kuna ibada tatu, ambayo ya kwanza
inaanza saa 12.00 asubuhi, ibada ya pili inaanza saa 1.00 asubuhi na ibada ya
tatu inaanza saa 4.00 asubuhi
No comments: