Mungu anahitaji umpende kwa nguvu na kwa bidii kubwa .Mungu
anahitaji kuona ziada ya upendo wako kwake.
Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika Usharika wa
Mwenge wa Kanisa la K.K.K.T mchungaji Elieza Mchomvu (pichani juu) alisema bidii
yako ya kumtafuta Mungu itakuwezesha kumpata , na ukimpata Mungu atakupa
utajiri wa heshima na atakubariki kazi za mikono yako na kila unachokifanya
Mungu anasema utajiri na heshima ziko mikononi mwake Zab: 24:1
Nchi na vyote vijazavyo ni mali ya bwana, dunia na wote
wakaao ndani yake
1 Petro 4: 10
Petro anasema tuwe mawakili wema mbele za bwana
Tunza uwakili wako kwani siku ya mwisho tutaulizwa ;
tulifanya nini katika dunia hii
Tunatakiwa tumtolee Mungu kw ahiari kwani tulivyo navyo sisi
ni mawakili tu;na ametuthamini sana kukupa mali yake ili uitunze
Mungu anataka tuhudumiane na kusaidiana sisi kwa sisi
alisisitiza mchungaji Mchomvu
Kila tulitendalo katika dunua hii, Mungu anaweka rekodi yako
mbinguni
1 Nyakati 29: 14
Kumtolea Mungu bila kushurutishwa tena kumtolea Mungu kwa
hiari yako na kwa moyo wako wote.Tujifunze kutoa kwa bidii, kwa kiasi, na wala
si kwa lazima
Usilazimishwe kutoa ila toa kwa hiari ili Mungu aweze
kukubariki
Musa, alitoa fungu la kumi, Abraham, Daudi nk. Nao
walimtolea Mungu na Mungu aliwabariki
Kuacha kumtolea Mungu fungu la kumi ni kumwibia Mungu na ni
laana kwako
Ukimtolea Mungu kwa uaminifu, Mungu anakuwekea ulinzi au
kinga katika maisha na mali zako zote
alimaliza mahubiri yake mchungaji Mtomvu
Malaki 3:11
Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi
No comments: