Latest News


More

BARAZA LA WAZEE LAVUNJWA RASMI USHARIKA WA MWENGE WA KANISA LA K.K.K.T

Posted by : Unknown on : Monday, August 25, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :
Ibada ya jumapili ya jana pamoja na mambo mengine ilikua maaluma kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa viongozi wa kanisa (baraza la wazee) ambapo ulifanyika takribani Katika Sharika zote za kanisa la K.K.K.T Dayosisi ya Mashariki na Pwani
Akizungumza kwenye ibada hiyo Usharika wa Mwenge mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi, alisema kabla ya kufanya uchaguzi ni budi kuvunja baraza lililopo hivyo washarika walikaa kama mkutano mkuu na kuwashukuru wazee waliohudumu kwa miaka minne kwenye Usharika huo
Baada ya sala ya kuwashukuru kwa huduma yao hiyo washarika walifanya uchaguzi kwa kufuata jumuiya moja baada ya nyingine kwa kuwasimamisha wale wate waliopendekezwa.

Pichani juu katibu wa baraza la wa zee wa Usharika wa Mwenge Mzee Kombe akimshika mkono mchungaji kwa niaba ya wazee wenzake baada ya kumaliza mda wa kutumika kwa miaka minne

Wazee wa kanisa wanaomaliza muda wao wakiwa mbele ya madhabahu  jumapili hiyo




No comments:

Leave a Reply