Watalii mbalimbali wakitazama mti huo
Vito vya thamani vikiwa vimepamba mti huo watalii wa ndani nao wakishangaa mti huo wa Christmas
Vito vya thamani vikiwa vimepamba mti huo watalii wa ndani nao wakishangaa mti huo wa Christmas
Watalii mbalimbali wakiwa wanapata picha ya pamoja kama ukumbusho kwenye mti huo wa aina yake
Mti wa Christmas maarufu kama Christmas tree umekua ukitumika kwa karne nyingi sasa kama pambo la litumikalo wakati wa sikukuu ya Christmas .Sikukuu hii ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo (kwa wakristo) hupambwa na mti huu maalum.Wakristo na hata wasio wakristo majumbani, maofisini, mahotelini hupenda kutumia mti huu kwa ajili ya kupendezesha maeneo yao ya bishara au hata majumbani mwao.
Huko Uarabuni kwenye hoteli moja ya kitalii wameamua kupamba mti wao kwa kutumia dhahabu na vito vya thamani ambavyo thamani yake ni kama dola milioni 11 sawa na fedha za kitanzania 16,335,000000 kama unavyoonekana katika picha hapo juu.Hakika mti umependeza.
Je wewe umeshanunua mti wako wa Christmas.Kama bado waweza agiza kwa mpambaji wa Abu Dhabi
Week end njema