Kanisa ni mahali ambapo Wakristo wanakutana kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu.Mara nyingi mfumo wa ujenzi unatofautiana kati ya kanisa na kanisa na kati ya dhehebu na dhehebu
Hapa nakuletea jumla ya makanisa 10 makubwa duniani kutoka kwenye madhehebu mbalimbali uya Kikristo
10. Sanctuary of Our Lady of Liche?, Poland
The Sanctuary of Our Lady ni kanisa kubwa kuliko yote nchini Polandna la 7 kwa ukubwa barani Ulaya .Kanisa hili lilianza kujengwa mwaka 1994 mkapa 2004.
9. Basilica of Our Lady of Peace, Ivory Coast
Kanisa la Basilica of our Lady of Peace of Yamoussoukrola nchini Ivory Coast ,ni kanisa la Roman Catholic na limetajwa kwenye kitabu cha Guinness World Records kama kanisa kubwa kuliko yote duniani. Liko kwenye eneo la 30,000 square meters (322,917 sq ft),na linachukua idadi ya waumini 18,000 kwa wakati mmoja.Kanisa hili la Basilica lilijengwa kati ya mwaka 1985 na 1989 na lilizinduliwa mwaka 1990 na Pope John Paul II.
8. Basilica of the Sacred Heart, Belgium
Hili ni kanisa la nchini Beligium linaloitwa National Basilica of the Sacred Heart likiwa ni kanisa la Roman Catholiclikiwa kwenye Parish inayoitwa Brussels, Belgium. Mfalme King Leopold II aliweka jiwe la msingi mwaka 1905wakati wa siku yake ya kukumbuka siku ya uhuru wa nchi hiyo kutimiza miaka75.Ujenzi wake ulisimama baada ya vita ya pili ya dunia a baadaye kuendelea tena na ujenzi na kumalizika mwaka 1969.
7. Milan Cathedral, Italy
Milan Cathedral (Duomo di Milano) nalo linasemekana ni kanisa kubwa kuliko yote duniani.Kanisa hili lilianza kujengwa mwaka 1386 na kumalizika 1965. Lina uwezo wa kuchukua waumini 40,000 people. Ni mojawapo ya kanisa kubwa la Gothic cathedral duniani na mojawapo ya kanisa maarufu barani Ulaya.
6. Church of the Most Holy Trinity, Portugal
Kanisa la Church of the Most Holy Trinity ni la nne kwa ukubwa kwa makanisa ya Katoliki na la sita kwa makanisa ya Kikristo duniani. Kanisa hili lilijengwa kati ya mwaka 2004 mpaka 2007 na likazinduliwa rasmi October 12, 2007. Lina uwezo wa kuchukua waumini 9,000 kwa wakati .
5. Liverpool Cathedral, United Kingdom
Kanisa la Cathedral Church of Christ la Liverpool, England ni la tano kwa ukubwa duniani.Kanis ahili liko kwenye eneo la 103,334 square feet (9600 square meters) na eneo kubwa la kanisa hili limejengwa kwa mawe. Kengele ya kanisa hili ni kubwa kuliko zote duniani na imepewa jina Barttlett Bells.
4. Cathedral of Saint John the Divine, United States
Kanisa la Cathedral Church of Saint John the Divine lililoko kwenye mji wa New Yorklinasemekana ndilo kubwa kuliko yote kwa makanisa ya Anglikan na la nne kwa ukubwa kwa makanisa ya Kikristo duniani. .
3. Cathedral of Seville, Spain
Kanisa hili pia linajulikana kama Catedral de Santa Maria de la Sede (Cathedral of Saint Mary of the See), Kanisa hili lilianza ujenzi wake mwaka 1402 na kuendelea mkapa kwenye karne ya 16.Liko kwenye eneo la sq m.11,520
\
2. Basilica of the National Shrine of Our Lady of Aparecida, Brazil
Kanisa hili la The new Basilica of the National Shrine of Our Lady of Aparecida lilijengwa mwaka 1955 lina uwezo wa kuchukua waumini 45,000 . Pope John Paul aliliita kanisa hili kama kanisa maalum nchini Brazil.
1. St. Peter’s Basilica, Vatican City
Hili ni kanisa kubwa kuwahi kuwepo duniani.Liko nchini Italy kwenye mji wa Roma.Lina uwezo wa kuchukua waumini mpaka 60,000. Kanisa hili la Basilica lilianza kujengwa mwaka 1506 mkapa 1626 na Michelangelo mmojawapo wa wasanifu wakubwa wakati huo wa majengo.
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: