Latest News


More

Njaa inavyotafuna wananchi wa Afrika

Posted by : Unknown on : Friday, July 29, 2011 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Njaa inaonekana kuwa tatizo sugu sana na inaua watu wengi Afrika sasa hivi.
Nchini Swaziland nchi ambayo ina idadi kubwa ya wagonjwa wa Ukimwi, waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi kwa kukosa chakula wameanza kula kinyesi cha ng'ombe kabla ya kumeza dawa hizo za kurefusha maisha

Kwa mujibu wa wanaharakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya yukimwi ilisema njaa ni tishio katika nchi hiyo hivyo kusababisha wagonjwa hao kula kinyesi cha wanyama

Swaziland ni mojawapo ya nchi zenye waathirika wengi wa H.I.V duniani.Nchi hiyo yenye jumla ya wakaazi milioni 1.2 lakini watu 230,000 ni waathirika wa gonjwa hilo

Siku chache zilizopita wamia ya wakaazi wa mji wa Mbabane waliandamana wakipinga hali ngumu ya uchumi inayoikabili nchi hiyo.